Klabu ya Yanga SC ya jijini Far Es Salaam
imejikuta katika wakati mgumu wa kutetea ubingwa wake baada yakufungwa
2-1 na Mgambo JKT huko jijini Tanga
. Dakika ya Kwanza Mgambo JKT
walipata goli la kuongoza kupitia kwa Fully Maganga.
Mohamed Neto
anatolewa nje baada ya kujihusisha na imani za kishirikina mchezoni,
hadi mapumziko Mgambo walikuwa mbele kwa goli moja. Dakika ya 50,
Nadir Haroub "Cannavaro" alisawazishia Yanga bao la kwa njia ya penati
baada ya Mgambo kufanya madhambi eneo la hatari.
Mgambo
walijihakijishia nafasi yakubaki ligi kuu baada yakujipatia bao la pili
dakika ya 69 kwa njia ya penati baada ya wapinzani wao kufanya madhambi,
na mpigaji wa penati hiyo Malima Busungu kutofanya ajizi.Hadi
kipenga cha mwisho Mkwakwani Tanga, Mgambo JKT 2 Yanga SC 1. Kwa matokeo
hayo klabu ya Yanga imezidi kushika nafasi ya pili katika msimamo ligi
kuu Tanzania Bara kwa pointi zao 46.
YANGA YAZIDI KUUWEKA UBINGWA WAKE REHANI

No comments: