
katika mechi ya La Liga kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid.
Bao moja la Barcelona lilifungwa na Iniesta katika dakika ya saba na Messi akafunga hayo matatu, mawili yakiwa ya mikwaju ya penati huku beki Sergio Ramos akilambwa kadi nyekundu kwa kumuangusha Neymar. Mabao matatu ya Madrid yalifungwa na Cristiano Ronaldo kwa mkwaju wa penati na Karim Benzema akapachika mawili.
Madrid wamebaki na pointi 70 sawa na Atltetico Madrid huku Barcelona wakifikisha 69 na kujisogeza vizuri kwenye mbio za ubingwa wa La Liga.
No comments: