Klabu ya Azam imeendelea kuutolea udenda ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara ya kuwafunga goli 1 kwa 0 Maafande wa JKT Oljoro jioni hii katika Uwanja wa Azam Complex,


ni John Bocco aliyepeleka pointi hizo 3 baada yakupiga shuti kali dakika ya 70 kipindi cha pili. Matokeo hayo yanaifanya Azam FC itimize pointi 47 baada ya kucheza mechi 21, mbele ya Mabingwa watetezi Yanga SC kwa pointi 4 lakini wakiwa na mechi moja mkononi baada ya kucheza michezo 20.
Wakati huo huo Coastal Union wameangalia makosa yao mchezo uliopita na kufanikiwa kumfunga Simba SC goli 1 kwa 0. Hadi mapumziko, tayari Coastal walikuwa mbele kwa bao hilo 1-0 lililofungwa na beki wa kulia Hamad Juma dakika ya 44
MATOKEO MENGINE
Mgambo JKT 1-1 Mtibwa Sugar
Ruvu Shooting 2-0 Ashanti United
No comments: