Watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na baadhi ya waandishi wa habari
wakipanda kwenye boti ndogo kwa ajili ya kuelekea kwenye kisiwa cha
Bongoye kufanya mkutano.
Frank Mvungi- Maelezo
Serikali imetenga Shilingi Bilioni 1.9 kwa ajili ya ruzuku kwa wavuvi katika kipindi cha mwaka wa Fedha 2013/14 ili kusaidia kukuza sekta ya uvuvi hapa nchini Hayo yamesemwa na Msemaji wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Mohammed Bahari wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam. Dkt Bahari amesema kuwa ruzuku hiyo itatolewa kwa kuzingatia vigezo ikiwemo waombaji kuwa na vyama vya ushirika na vilivyosajiliwa kisheria. Alitaja vigezo vingine kuwa ni chama cha ushirika kiwe kinafanya kazi za uvuvi kufuatana na sheria ya uvuvi na 22 ya mwaka 2003 na kanuni za uvuvi za mwaka 2009 na miongozo mbalimbali.
Aliongeza kuwa chama hicho kiwe na akaunti benki iliyo hai na kithibitishe kuwa na uwezo wa kuchangia asilimia 40% ya gharama ya mradi husika, ambapo Serikali itachangia asilimia 60% ya gharama ya mradi husika. “Chama husika kitapitisha maombi yao kwa Mkurugenzi wa Halmashauri husika kwa ajili ya kupitia maombi hayo na kuona kama yanakidhi vigezo viliwekwa na baada ya hapo kuwasilishwa Wizarani” alisema Dk. Bahari.
Watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa wamefika kwenye kisiwa cha Bongoye.
Alisema
miradi itakayofadhiliwa ni pamoja na ununuzi wa boti za uvuvi, injini
na vifaa vingine vitakavyowawezesha wavuvi kuongeza tija katika shughuli
za uvuvi
Dkt
Bahari alifafanua kuwa ruzuku hiyo kwa wavuvi itakuwa na manufaa
makubwa kama vile kuongeza mapato ya wavuvi na wafanyabiashara wa mazao
ya uvuvi.
Aliongeza
kuwa ruzuku hiyo pia itaongezeka maduhuli ya Serikali, kupunguza
vitendo vya uvuvi haramu,kuimarika kwa biashara ya mazao ya uvuvi na
kuongeza ajira katika sekta ya uvuvi. Naye
Mkurugenzi Msaidizi Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi, Baraka Mngulwi
alitoa wito kwa wale wote wanajihusisha na vitendo vya uvuvi haramu
kuacha tabia hiyo mara moja kwa kuwa Serikali imeimarisha doria katika
maeneo yote .
Aliongeza
kuwa kwa wale wanatumia nyavu ambazo zimepigwa marufuku nao waache
mara mara moja tabia hiyo na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa
wale wote watakaokwenda kinyume cha sheria ya uvuvi na. 22 ya mwaka 2003
na kanuni zake za mwaka 2009.
Alizihimiza
Halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa sheria za uvuvi na kanuni zake
zinazingatiwa kikamilifu na kuwa uvuvi haramu na biashara ya samaki
wachanga vinadhibitiwa katika maeneo yao.


Msemaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk. Mohammed Bahari akizungumza na waandishi wa habari juu ya ruzuku kwa wavuvi.Katikati ni Afisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) Frank Mvungi na mwisho ni Mkurugenzi Msaidizi wa Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi, Baraka Mngulwi.





No comments: