ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5

 Hii ndiyo hali halisi, baada ya mvua kunyesha hii leo mkoani Njombe, kituo hicho kimegeuka matope matupu, na kusababisha watumiaji wa kituo hicho kupata tabu ya kutembea kwa shida na kutafuta eneo la kukanyaga ili wapite. Kamera yetu imeshuhudia abiria wakikanyaga matope na madimbwi ya maji machafu yaliyoshamiri kituoni hapo huku pia wakirushiwa maji machafu na magari kituoni humo
Hali halisi ndiyo hii.
 Abiria ambaye jina lake halijajulikana mara moja akipita kwenye matope yaliyosheheni kwenye kituo hicha cha mabasi Njombe.
Ni mwendo wa kuchagua eneo la kukanyaga, wengine wanapandisha suruali zao juu zisipate matope.

 Huwenda upande huu unaafadhali kwa abiria hawa lakini wapi, tope tuu.
Tope

Licha ya tabu hii inayowakumba watumiaji wa kituo hiki cha mabasi Njombe, ushuru umekuwa ukikusanywa kama kawaida, lakini miezi michache iliyopita halmashauri ya Njombe ilitangaza kuwa haina mpango wa kukikarabati kituo hicho na badala yake imetenga eneo lingine kwa ajili ya kujenga kituo kipya cha mabasi.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment


Top