Klabu ya Manchester City imeendelea kupunguza nafasi ya pointi baada ya kumfanyia roho mbaya jirani yake, Man U kwa kumfunga magoli 3-0 usiku huu katika Uwanja wa Old Trafford.
Man City ilianza kujihakikisha kuchukua pointi 3 dakika ya 1 baada ya mpira uliopigwa na Samir Nasri kugonga mwamba na kumkuta mfungaji, Edin Dzeko.
Bahati ilizidi kumuangukia Dzeko baada ya kufunga goli la Pili dakika ya 56 kwa kunganisha kona iliyopigwa na Nasri. Yaya Toure alihitmisha karamu ya mabao dakika ya 90 kwa shuti safi lililomshinda mlinda mlango wa Man U.
Kwa matokeo hayo Man City wanapanda hadi nafasi ya pili katika msimamo na pointi zao 66.
UJIRANI WA MASHAKA, CITY YAFANYA KWELI MACHINJIONI

No comments: