Klabu ya Arsenal imeshindwa kuutumia uwanja wake wa nyumbani baada yakulazimishwa sare ya magoli 2 kwa 2 na Swansea City. Swansea ilikuwa ya kwanza kupata goli kupitia Wilfried Bony dakika ya 11 kipindi cha kwanza na kupelekea kudumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa kupooza ndipo Meneja wa Arsenal kufanya mabadiliko ya kumtoa Chamberlain na kuingia Podolski, dakika ya 73 aliisawazishia timu yake goli hilo. Dakika moja baadae Giroud akaiandika Arsenal goli la Pili kwa kumalizia pande la Podolski.
Arsenal ikiwa imeamini imejihakikishia kuondoka na pointi 3 hali ilikuwa tofauti baada ya Flamini kujifunga dakika ya 90 baada ya Leon Britton na Angel Rangel kugongea vizuri eneo la hatari. Kwa matokeo hayo Arsenal inaendelea kubaki nafasi ya Nne katika msimamo
MATOKEO MENGINE
Newcastle United 0 Everton 3
BAADA YA 6 ARSENAL YAAMBULIA SARE

No comments: