ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5

 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana toka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo James Kajugusi akiongea na Vijana (Hawapo pichani) Waliohudhuria katika kongamano la vijana wa Vyuo vya elimu ya juu kuhusu wajibu wa vijana katika kuimarisha muungano miaka 50 tangu kuzaliwa kwake.
 Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ruaha Prof. Gaudens Mpangala akiongea na vijana( Hawapo pichani) kuhusu wajibu wao katika kuimarisha na kuendeleza muungano wa tanzania baada ya miaka 50 na kuwataka vijana wa Tanzania kufanya utafiti na uchambuzi wa kina zaidi kuhusu utaifa katika majukumu yao ya kuimarisha na kuendeleza Muungano wa Tanzania.
  Prof. Issa Shivji akiwaeleza vijana( Hawapo pichani) na kuwataka vijana kutambua kuwa wote wamezaliwa wakiwa Watanzania, utaifa wao ni Utanzania, Utambulisho wao ni Utanzania, wanajitambue kama Watanzania na wanatambuliwa na wengine kama Watanzania.Wakati wa Kongamano la Vijana.
Baadhi ya Vijana waliohudhuria kongamano la vijana kuhusu wajibu wa vijana katika kuimarisha muungano miaka 50 baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
 Mwanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Peter Magoti akiongea na Vijana waliohudhuria kongamano hilo na Kuwataka kuwa wamoja na kuhakikisha wanaulinda na kuuenzi muungano wa Tanzania kwa Miaka mingi zaidi.
Katibu hamasa Taifa wa Umoja wa vijana CCM Paul Makonda akiwaeleza Jambo Vijana wakati wa Kongamano la Vijana Lililofanyika Jijini Dar Es Salaam.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment


Top