Klabu ya Yanga imewafanya mbaya Maafande, Tanzania Prisons ya Mbeya
kwa kuifunga magoli 5-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Ushindi
huo unaifanya Yanga kutimiza pointi 46 baada ya mechi 21, ikizidiwa
pointi nne na Azam FC walio kileleni.
Emmanuel Okwi aliifungia Yanga bao la kwanza dakika ya 20 kwa mpira wa adhabu baada yakufanyiwa madhambi nje kidogo na eneo la hatari, dakika ya 33 Yanga ilifanya mabadiliko kwa kumtoa Jerryson Tegete na nafasi yake kuingia Hussein Javu.
Mabadiliko hayo yalikuwa na manufaa kwa yangu dakika 4 mbele Javu alipiga krosi na Mrisho Ngasa akaweka mpira kimiani na kupeleka ubao kusoma 2-0. Prisons walipata penalti kutokana na Oscar Joshua kucheza rafu lakini Lugano Mwangama akapaisha. Hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa magoli 2-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi, dakika ya 60 alitoka Okwi nafasi yake ikachukuliwa na Hamis Kiiza na dakika ya 68 Kiiza akafunga goli la 3. Dakika ya 76 Nahodha wa Yanga anaipatia goli la 4 kufuatia Hussein Javu kuangushwa eneo la hatari.
Hamis Kiiza alihitimisha karamu ya magoli baada yakuonganisha krosi dakika ya 88 na kupeleka kicheko Jangwani
YANGA YAWAPA DALA MAAFANDE

No comments: