Mabingwa hao wa Uhispania wamefungiwa kufanya usajili wowote kwa muda wa miezi 14 baada ya kuvunja sheria ya usajili wa wachezaji chini ya umri wa miaka 18.
Klabu hiyo toka Catalan haitoweza kununua wala kuuza wachezaji mpaka msimu wa kiangazi wa mwaka 2015 baada ya kufungiwa kwa kipindi cha misimu miwili ijayo. Kama vile haitoshi FIFA imeipiga faini ya euro 305,000 klabu hiyo. Huku pia ikilipiga faini ya euro 340,000 Shirikisho la soka la nchini humo ( RFEF ) kwa kosa la ukiukwaji wa kanuni hiyo.
No comments: