
Chanzo cha maji Luhira ambacho wakulima wanafanya uchafuzi kwa kupulizia kemikali za sumu kwenye mashamba yao ya nyanya.
Watu wanaoishi katika Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma wapo katika hatari ya kukumbwa na magonjwa mbalimbali na hata kupoteza maisha kutokana na kutumia maji ya Mto Luhira ambao umechafuliwa kwa kemikali mbalimbali.
Luhira ni chanzo cha Mto Ruhuhu ambao unamwaga maji yake Ziwa Nyasa. Mto Luhira unaanzia kwenye Milima ya Matogoro iliyopo nje kidogo ya Mji wa Songea, milima hiyo pia ni chanzo cha mito Ruvuma na Luegu ambayo inamwaga maji yake Bahari ya Hindi.
Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Songea (SOUWASA) inategemea chanzo cha maji cha Mto Luhira kwa ajili ya kusambaza maji kwa wakazi zaidi 180,000 wa Mji wa Songea.
Katika chanzo hicho wakulima wanalima nyanya, karoti, Chinese, spinachi, mboga za maboga pamoja na mboga nyingine ambapo hupulizia madawa ya kuuwa wadudu waharibifu ambayo ni hatari kwa afya na baadhi yake yamepigwa marufuku kimataifa yakiwemo blue-copper, red-copper, DDT na kimatila.
Wengi wanaathirika na maji ya sumu
No comments: