ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5

 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kulia) akipokea ufunguo ikiwa ishara ya kukabidhiwa magari matano kutoka kwa Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada wakati wa tafrija fupi ya makabidhiano ya magari hayo kutoka Serikali ya Japan kwa ajili ya kusaidia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika majukumu yake ya kuzima moto na uokoaji nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto Kanda ya Ilala, jijini Dar es Salaam.  
                            
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kulia) na Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada wakikata utepe ikiwa ishara ya makabidhiano ya magari matano yaliyotolewa na Serikali ya Japan kwa ajili ya kusaidia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini. Magari hayo yamekabidhiwa katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto Kanda ya Ilala, jijini Dar es Salaam.

                              
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akiiwasha moja ya magari matano yaliyotolewa na Serikali ya Japan kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Magari hayo matano yalitolewa na Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada wakati wa tafrija fupi ya makabidhiano ya magari hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto Kanda ya Ilala, jijini Dar es Salaam.
                              
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali Pius Makuru Nyambacha akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (katikati) ili aweze kuzungumza na baadaye kukabidhiwa magari matano ya kuzima motona uokoaji. Magari hayo yametolewa na Serikali ya Japan kupitia balozi wake nchini, Masaki Okada (kushoto) katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto Kanda ya Ilala, jijini Dar es Salaam.
                                 
Sehemu ya magari matano yaliyokabidhiwa na Balozi wa Japan, Masaki Okada kwa niaba ya Serikali yake. Magari hayo matano yaliyotolewa kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yalipokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto Kanda ya Ilala, jijini Dar es Salaam. 

PICHA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment


Top