ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5

 Mabomba yaliathirika baada ya mvua kubwa iliyonyesha mwishoni mwa wiki eneo la Jangwani.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Bashir Mrindoko (wa pili kulia) akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Jackson Midala (wa kwanza kushoto) walipotembelea eneo la Jangwani

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Bashir Mrindokoleo ametembelea eneo la Jangwani, Darajani, barabara ya Morogoro kujionea uharibifu mkubwa wa mabomba ya maji.

Mabomba hayo ya inchi 16 yenye urefu wa mita 12 yamezolewa na maji kutokana na atharii liyoletwa na mvua kubwa ya mwishoni mwa wiki inayoendelea jijini Dar es Salaam.

“Ni athari kubwa ambayo imesababishwa na mvua hii na mpaka kukata mabomba ya maji, ni muda mrefu tangu mvua ya aina hii kutokea Dar es Salaam”, alisema Inj. Mrindoko.

“Nimekuja kuangalia hali halisi na kuona namna gani tutafanya kufanya ukarabati wa mabo mba haya, ili kurudisha huduma ya maji kwa maeneo yaliyoathirika baada ya tukio hili. Tumefanya tathmini na kuona nini cha kufanya na utekelezaji utaanza mara moja”, aliongeza Inj. Mrindoko.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment


Top