ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5


Matumaini ya Asernal kufuzu kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao yameanza kufufuka baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya West Ham kwenye mchezo wa ligi kuu soka nchini England uwanja wa Emirates.
Lukas Podolski amefunga mabao mawili katika dakika ya 44 na 78, huku moja likifungwa na Olvier Giroud dakika ya 54. West Ham walikuwa wa kwanza kufunga leo hii katika dakika ya 40 kipindi cha kwanza kupitia kwa Matthew Jarvis .
Mashabiki wa Asernal huwa hawana imani kubwa na Giroud na katika mchezo wa leo alikosa nafasi kadhaa kipindi cha kwanza, lakini wakati mashabiki wakijiuliza kama mshambuliaji huyo anaweza kuwa tegemeo kwa siku za usoni, alifunga bao muhimu mno katika ushindi huo. Umuhimu wa bao la Giroud unatokana na uhitaji mkubwa wa Asernal kufuzu michuano ya UEFA msimu ujao.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment


Top