ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5


Siku mbili baada ya kumalizika kwa mashindano ya kutafuta klabu bingwa wa taifa wa mpira wa kikapu nchini Tanzania, baadhi ya makocha waliokuwa wanazinoa timu zao katika michuano hiyo pamoja na wachezaji wamefurahishwa na juhudi za Uongozi wa shirikisho ulioingia madarakani hivi karibuni kwa kuongeza idadi ya timu zilizoshiriki michuano hiyo.

Makocha Joseph wa savio na Bakari wa timu ya Bandari ya jijini Tanga pamoja na Nahodha wa Savio, Roman Anania wamesema michuano ya mwaka huu imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na ushiriki wa timu nyingi katika michuano hiyo. Wakati huo huo, Katibu mkuu wa Shirikisho la Mpira wa kikapu Tanzania TBF Salehe Zonga amesema wapo mbioni kuanza mchakato wa kutafuta vijana watakaoshiriki katika michuano mbalimbali ya kimataifa yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni jijini Kampala nchini Uganda.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment


Top