Mchezaji Delgado alikuwa shujaa wa FC Basel baada yakufunguka mara
mbili katika ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Valencia hatua ya robo
fainali raundi ya kwanza. Alifunga magoli hayo dakika ya 34 na 38
kipindi cha kwanza, hadi timu zinaenda mapumziko Basel walikuwa mbele
kwa magoli 2-0.
Valencia akiwa amekubali kufungwa ugenini, wenyeji walifanya mashambulizi dakika za lala salama na kufanikiwa kupata bao la 3 kupitia Stocker katika dakika za nyongeza baada ya 90 kumalizika. Kwa matokeo hayo itawalazimu Valencia kushinda 4-0 katika mechi ya marudiano wiki ijayo.
MATOKEO: FC BASEL YATANGULIZA MGUU MMOJA NUSU FAINALI, YAWAPIGA 3-0 VALENCIA

No comments: