Klabu ya PSG imeutumia vyema uwnja wake wa nyumbani baada kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Chelsea, Lavezzi alianza kuwaandikia goli matajiri hao wa Paris dakika ya 3 tu ya mchezo.
Dakika ya 27 Hazard aliisawazishia timu yake kwa mkwaju wa penati baada ya Thiago Silva kumfanyia madhambi Oscar eneo la hatari. Hadi wanaenda mapumziko timu zilikuwa 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na kushambuliana kwa kushtukiza hadi kupelekea wenyeji kupata goli la pili dakika ya 62 kwa mpira wa adhabu uliomgonga Luiz katika harakati za kuokoa.
Kiungo aliyesajiriwa kwa fungu kubwa mara baada ya timu kuchukuliwa na matajiri, Pastore alipigilia msumari wa mwisho dakika za lala salama na kupuelekea matokeo kuwa 3-1.
MATOKEO: PSG YAMKAMUA 3-1 CHELSEA

No comments: