
Unaweza kuichukulia kivyovyote lakini maandishi ya member wa Tamaduni
Music, Nash MC yameeleza wazi kuwa anamzimia mrembo na mwimbaji wa
kundi la Shosteez, Meninah la Diva.
Comment ya Nash MC aliyoiweka kwenye post ya Jabir Saleh a.k.a Kuvichaka aliyokuwa ameweka kwenye ukurasa wa Facebook akiwa na Dayna Nyange ambaye atakuwa mkali wa The Jump Off kuanzia wiki ijayo, ilikuwa na ujumbe wa wazi kwa mtangazaji huyo. “Siku ukimhoji menina nistue maana namzimia kweli.” Aliandika Nash MC.
Hata hivyo, ujumbe huo haukuishia kwa Kuvichaka na akaupeleka kwa watu wengine ambao wanaweza kukutana na Meninah au wale ambao walidhani ametereza tu kuandika kwa uwazi.
“Hilo lipo wazi na mkimuona mwambieni.” Alisisitiza Nash MC.
Rapper huyo wa Naandika alijitoa kwenye lawama binafsi na kuchombeza kiutani kuwa kilichomsukuma ni upendo. “Sio mm ni sababu ya mapendooooooo!” AAYAAAAAAA
No comments: