ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5

Rwanda inaadhimisha miaka 20 tangu kutokea mauaji ya kimbari mwaka 1994
Watu laki nane waliuawa wengi wakiwa wa kabila la Tutsi na Wahutu wenye msimamo wa kadri. Wote waliuawa na watutsi wenye msimamo mkali.
Hii leo Rais Paul Kagame anatarajiwa kuwasha mwenge ambao utasalia hivyo kwa siku 100 , kipindi ambacho mauaji ya kimbare yalifanyika.
Mgogoro wa kidiplomasia umesababisha Waziri wa sheria wa Ufaransa, kujiondoa katika shughuli za kumbukumbu ingawa Ufaransa inasema kuwa balozi wake ataiwakilisha nchi hiyo.
Wengi wa waathiriwa wa mauaji ya Rwanda, walishambuliwa kwa mapanga kwa siku 100. Mauaji hayo yalianza Aprili mwaka 1994, punde baada ya kufariki kwa hayati Rais Juvenal Habyarimana.
Alifariki wakati ndege yake iliposhambuliwa katika anga ya Kigali na kudunguliwa.
Baadhi ya viongozi wa kidini walihusishwa na ghasia zilizofuata kifo cha Habyarmana.
Mauaji ya kimbari yaliisha mwezi Julai 1994 wakati chama cha RPF, kilichokuwa cha waasi wa Tutsi wakati huo, kilipoingia nchini humo kutoka Uganda na kuchukua uongozi wa nchi hiyo.

Kumbukumbu zinaanza kwa kuwekwa mauwa katika eneo la kumbukumbu ya mauaji hayo na kufuatiwa na kuwashwa kwa mwenge katika uwanja wa michezo wa Amahoro mjini Kigali.

Mwenge huo umekuwa ukitembezwa katika nchi hiyo kwa miezi mitatu iliyopita
Viongozi wa kimataifa akiwemo waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair,aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki na katibu mkuu wa UN Ban Ki-moon wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo.
Mnamo Jumapili mamia ya watu walihudhuria maombi kuwakumbuka maelfu
 waliouawa 




Mauaji ya kimbari Rwanda
6 Aprili: 1994: Rais Habyarimana afariki katika ajali ya ndege
7 Aprili: Wanajeshi wa Rwanda pamoja na waasi wawaua wananchi
8 Aprili:Kundi la waasi la (RPF) laanza kupambana
11 Aprili: Maelfu wauawa
17 Mei: Baraza la usalama la umoja wa mataifa lasema mauaji ya kimbari yametokea
22 Mei: RPF yadhibiti uwanja wa ndege wa Rwanda
22 Juni: Mauaji ya watutsi yaendelea licha ya kuwepo wanajeshi wa Ufaransa nchini humo
4 Julai: RPF yadhibiti Kigali

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment


Top