
Waziri wa
Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka
kwa Ofisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Carloyne Newa (kushoto), kuhusu kujiunga na Mfuko huo wakati wa uzinduzi
wa michuano ya Kombe la NSSF kwa vyombo vya Habari. Michuano hiyo
inafanyika katika viwanja vya TCC Chag'ombe jijini Dar es Salaam.

Ofisa
Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Carloyne Newa
(kulia), akitoa maelezo kwa baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam walipofika
katika banda la NSSF, na kutaka kujiunga na mfuko huo, wakati wa
michuano ya kopmbe la NSSF kwa vyombo vya habari. Mkazi wa jijini Dar
es Salaam akiulizia taratibu za kujiunga na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa
NSSF.

Ofisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Carloyne Newa (kulia), akitoa maelezo kwa baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam walipofika katika banda la NSSF.

Maofisa wa NSSF wakitoa ufafanu kuhusu mafao yanayotolewa na Shirika hilo.

Mwanachama mpya aliyejiunga na Shirika la taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), akijaza fomu ya kujiunga na mfuko huo.

Baadhi ya waandishi wa wakipata maelezo kabla ya kujiunga na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF.
No comments: