Afisa Kazi wa
Wizara ya Kazi na Ajira Bw. Themistocles Rumboyo akiwaeleza waandishi wa habari
leo jijini Dar es Salaam kuwa hadi kufikia Februari mwaka huu jumla ya maombi
56 ya makampuni ya huduma za ajira nchini yamewasilishwa kwa Kamishna wa Kazi.
Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bw. Ridhiwani Wema.
Afisa
Kazi wa Wizara ya Kazi na Ajira Bw. Omari Sama akijibu swali la waandishi wa
habari waliotaka kujua taratibu za kusajili wakala binafsi wa huduma za ajira
hapa nchini. Kulia ni Mkuu wa Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini Bw. Ridhiwani Wema.
Afisa Kazi wa
Wizara ya Kazi na Ajira Bw. Themistocles Rumboyo akiwaeleza waandishi wa habari
leo jijini Dar es Salaam kuwa hadi kufikia Februari mwaka huu jumla ya maombi
56 ya makampuni ya huduma za ajira nchini yamewasilishwa kwa Kamishna wa Kazi.
Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bw. Ridhiwani Wema.
WIZARA YA KAZI NA AJIRA TAARIFA KWA UMMA
UTEKELEZAJI WA TAMKO LA SERIKALI
KUHUSU UENDESHAJI WA WAKALA BINAFSI WA HUDUMA ZA AJIRA NCHINI
1. Tarehe 27/1/2014, Wizara ya Kazi na Ajira
ilitoa Tamko la Serikali kuhusu uendeshaji wa Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira
nchini. Pamoja na mambo mengine Wizara imepiga marufuku Wakala kuajiri na
kukodisha wafanyakazi na kuwataka Wakala na kampuni zilizo katika utaratibu huu
ziwahamishie Wafanyakazi husika kwa Kampuni zilizokodishwa. Aidha, Wakala
waliagizwa wawasilishe upya maombi
ya usajili wa Uwakala kwa Kamishna wa
Kazi.
2. Hadi kufikia tarehe 28/02/2014, jumla ya maombi hamsini na sita (56) yamewasilishwa kwa Kamishna wa Kazi.
3. Aidha Kampuni au Wakala zilizoomba usajili tumewaarifu watupatie taarifa zifuatazo:
·
Katiba ya uendeshaji
na usimamizi wa shughuli za kampuni au Wakala (Memorandum&Articles of Assocition).
·
Hati ya usajili wa
kampuni (Certificate of incorporation).
·
Leseni ya Biashara(Business License).
·
Namba ya usajili wa
mlipa kodi (Tax identification Number).
·
Wasifu wa Kampuni au
Wakala pamoja na ujuzi na uzoefu wa
wataalamu au watumishi katika uendeshaji wa huduma za ajira(Company profile).
·
Uthibitisho wa
Kampuni au Wakala kama analipa kodi kwa mujibu wa taratibu(The current tax clearance letter from Domestic revenue/larger tax
payers department)
·
Anuani kamili ya
makazi(Permanent physical company address) n.k.
Wizara itazitumia taarifa hizi katika upekuzi,ufuatiliaji,ukaguzi na
utoaji uamuzi sahihi juu ya utoaji
vibali vya uendeshaji wa huduma za ajira nchini.
4. Baadhi ya Wakala tayari wamefuata agizo na wamesitisha utaratibu wa
kukodisha wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kuhamishia Ajira za wafanyakazi hao
kwenye Makampuni husika. Aidha, Mawakala wengine wameomba kuongezewa muda ili
waweze kukamilisha taratibu za kuhamisha wafanyakazi. Wizara imepitia kwa kina
maombi haya na imekubali kuongeza muda wa miezi
miwili kuanzia tarehe 28/02/2014.
5. Kufuatia upotoshwaji
unaofanywa na baadhi ya watu au makampuni kuhusiana na maudhui ya Tamko la
Serikali, Wizara inapenda kusisitiza yafuatayo.
i.
Kwamba, “Wakala
Binafsi wa Huduma za Ajira” inajumuisha
Mtu binafsi, Kampuni,Taasisi au chombo chochote kinachotoa huduma ya kuunganisha
watafuta kazi na waajiri pasipo wakala wa huduma za ajira kuwa sehemu ya
mahusiano ya kiajira yanayoweza kujitokeza baina ya watafuta kazi na Waajiri.
Pia, inajumuisha utoaji wa huduma zingine zinazohusiana na utafutaji kazi kama
vile kutoa ushauri nasaha wa ajira, kutoa taarifa za soko la ajira kwa watafuta
kazi na waajiri.
ii.
Kwamba, ukodishaji wa
huduma (outsourcing of services)
haujapigwa marufuku bali kilichopigwa marufuku ni ukodishwaji wa watu (outsourcing of persons). Hivyo ni
marufuku kwa Wakala wa huduma za Ajira kuajiri na kukodisha wafanyakazi, au
kuajiri kwa niaba ya kampuni nyingine na wakala hao kuwa sehemu ya mahusiano ya
ajira yanayoweza kujitokeza baina ya watafuta kazi na Waajiri.
6.
Mwisho, Wizara inapenda kusisitiza kuwa Mtu
yeyote anayetaka kufanya shughuli za
huduma za ajira hana budi kuzingatia taratibu na kanuni chini ya Sheria ya Kukuza Huduma za Ajira Na. 9 ya
1999.
IMETOLEWA NA
SAUL.H.KINEMELA
KAMISHNA WA KAZI
No comments: