Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy akizungumza kwenye mkutano na
waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu faida za Mtambo Maalum wa Kusimamia
Mawasiliano na Udhibiti wa Mapato yatokanayo na Simu unaojulikana kama
Telecommunication Traffic Monitoring System (TTMS). Mtambo huo unaweza kutambua
mawasiliano ya udanganyifu katika mitandao na namba za ulaghai zinazotumika
kwenye mawasiliano ya kimataifa kinyume cha sheria. Kulia ni Afisa Habari wa
Idara ya Habari Maelezo Bw. Frank Mvungi.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye
mkutano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uliofanyika jijini Dar es Salaam. Lengo la
Mkutano huo ni kuelezea mtambo wa TTMS unavyodhibiti udanganyifu katika
mitandao ya simu za kimataifa.
Naibu Mkurugenzi anayehusika na usimamizi
wa Mtambo Maalum wa Kusimamia Mawasiliano na Udhibiti wa Mapato ya Simu (TTMS)
kutoka TCRA, Mhandisi Sunday Richard akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari
jinsi mtambo huo unavyofanya kazi ya kudhibiti udanganyifu katika mitandao ya
simu za kimataifa zinazoingia hapa nchini.
No comments: