ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5



Muuguzi wa kituo hicho Pilly Ntongolo akionyesha jinsi stoo hiyo ya Madawa ya Binadamu ilivyochanganyika na Saruji





Muuguzi wa kituo hicho Pilly Ntongolo yeye ndie Daktari , Mtunza Ghala na Mkunga kazi ipo






                                         Hii ndiyo Zahanati yenyewe

                         Choo sikunyingi kimeziba ni pango la Mijusi na Nyoka sasa



Mgonjwa akisubiri huduma

Dawa zinazosambazwa na Serikali katika zahanati ya kijiji cha Malangali kata ya Totowe wilaya ya Chunya zipo hatarini kuharibika kutokana na utunzwaji mbovu.

Muuguzi wa kituo hicho Pilly Ntongolo amekiri kuwepo kwa tatizo hilo kwa muda mrefu tangu zahanati hiyo kuzinduliwa kwa mbio za mwenge miaka miwili iliyopita huku uongozi wa kijiji na kata kushindwa kuchukua hatua madhubuti.

Ntongolo amesema kuwa dawa hizo zimekuwa zikitunzwa hovyo kutokana na kutokuwepo kwa shelfu za mbao ambazo zingewezesha kupangwa kwa utaratibu unaoeleweka,lakini imekuwa tofauti baada ya uongozi wa kijiji kushindwa kununua mbao za kutengenezea shelfu hizo.

Hali imekuwa mbaya zaidi baada ya utaratibu mpya wa kusambaza dawa vijijini kupitia mpango wa shirika la Bohari na usambazaji dawa[MSD]kwa walengwa kuzambaza dawa katika zahanati hiyo kulundikwa hovyo bila utaratibu hali ambayo ina hatarisha usalama wa dawa hizo.

Uchunguzi umebaini kuwa kituo hicho chenye namba za MSD 105866 kuwa na tatizo pia na tatizo kubwa la kuharibika dari baada ya mchwa na popo kuharibu dari na kusababisha dawa hizo kumwagikiwa na vumbi pia na mikojo ya popo hali inayohatarisha afya za watumiaji wa dawa hizo.

Pia zahanati hiyo inakabiliwa na tatizo la kuwepo maji hali inayolazimu muuguzi huyo kulazimika kuchota maji kutoka kwake wakati wa kutoa huduma ya kuzalisha kwa wajawazito wanaofika kujifungua.

Aidha vyoo vya zahanati hiyo vimeziba kutokana na ukosefu wa maji hali inayolazimu wagojwa kujisaidia vichakani kutokana na kukosekana kwa maji hali inayohatarisha afya kwa wagonjwa.

Changamoto nyingine inayoikabili zahanati hiyo ni pamoja na mazingira machafu ambapo nyasi zimeota hadi katika upenu wa zahanati,ambapo muuguzi hulazimika kuacha huduma kwa wagonjwa ili kupunguza uchafu uliokithiri.

Mtendaji wa kijiji hicho Yaledi Mwanguku hakuwa tayari kumpeleka mwandishi katika zahanati hiyo akidai muuguzi hayupo ,lakini mwandishi alipokwenda alimkuta muuguzi hali inayoonesha kutokuwa tayari kujibia kero hii.

Hivi sasa zahanati hiyo haina Mwenyekiti wa Kamati ya Afya kutokana na Ahmed Ndauka kujiuzuru kutokana na tofauti baina yake na muuguzi ambapo Kamati ya Afya ya wilaya ilifika kutatua mgogoro huo.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment


Top