Watu 13 akiwemo askari wa kikosi cha usalama barabarani wamepoteza maisha baada ya kugongwa na basi la kampuni ya Sumry lililokuwa likitoka Kigoma kwenda Dar katika kijiji cha Ikungi mkoani Singida.
Ajali hiyo ilitokea baada ya ajali ya kwanza iliyolihusisha lori
lililomgonga mwendesha baiskeli aliyepoteza maisha papo hapo na wakati
wananchi wakiwa wamekusanyika eneo hilo la ajali huku trafiki akiendelea
kupima ajali hiyo, lilitokea basi la kampuni ya Sumry na kuwagonga watu
hao pamoja na trafiki na kupelekea jumla ya watu 14 kupoteza maisha
eneo hilo.
Basi hilo lililokuwa likitokea Kigoma kwenda Dar halikuweza
kusimama eneo hilo mpaka dereva wake alipokwenda kujisalimisha kituo cha
polisi Ikungi, Singida.
Miili 14 ya waliopoteza maisha katika ajali
hiyo imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Singida pamoja na
majeruhi wawili waliopelekwa hospitalini hapo.
Gari la polisi likiwa limepakia maiti zaidi ya kumi zikipelekwa hospitali ya mkoa wa singida kwa ajili ya kuhifadhiwa na kutambuliwa
PICHA ZOTE NA :Elisante Mkumbo-Singida
Moja ya maiti ya ajali ya basi la sumry iliyo tokea katika kijiji cha Utaho Wilayani Ikungi ikisubiri kupakiwa katika gari la polisi.
Baadhi ya miili ya wakazi wa kijiji cha Utaho wilaya ya Ikungi, waliogongwa na basi la Summry ikiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa wa Singida mjini humo.
Baadhi ya miili ya wakazi wa kijiji cha Utaho wilaya ya Ikungi, waliogongwa na basi la Summry ikiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa wa Singida mjini humo.
MUNGU AZILAZE ROHO ZA
MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!
No comments: