Mbeya City imelazimishwa sare ya bila kufungana na Ashanti United Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam hivyo kushindwa kuiengua Yanga SC nafasi ya pili pamoja na kuifikia kwa pointi. Sare hiyo inaifanya Mbeya City ifikishe pointi 46 sawa na Yanga SC, ambayo inaendelea kukaa nafasi ya pili kwa wastani mzuri wa mabao. Hata hivyo, Mbeya City imecheza mechi mbili zaidi ya Yanga. Ashanti ilimaliza mechi hiyo ikiwa pungufu, baada ya mchezaji wake Ally Abdallah kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 89 kwa kumchezea rafu Deogratius Julius.
Beki wa Ashanti United, Iddi Silas aliyeruka juu kupambana na mshambuliaji wa Mbeya City, Mwagane Yeya
Ashanti inayofundishwa na kocha mkongwe Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ ilicheza soka maridadi na kutawala sehemu ya kiungo muda wote wa mchezo, lakini wakashindwa kutumia vizuri nafasi walizotengeneza.
Deus Kaseke wa Mbeya City akimtoka Abuu Mtiro wa Ashanti United
Beki wa Ashanti, Shaffih Hassan akiruka kupiga kichwa dhidi ya Deus Kaseke wa Mbeya City na kushoto Hassan Kabunda akiwa tayari kutoa msaada
Hassan Mwasapili wa Mbeya City akimtoka Joseph Mahundi wa Ashanti kushoto
No comments: