ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5





Azam imeibwaga mabao 3-0 timu ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wake wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni hii.
Ushindi huo unaisogeza karibu kabisa na ubingwa wa Ligi Kuu Azam FC kwa kufikisha pointi 56 baada ya kucheza mechi 24, ikifuatia na mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 52 za mechi 24 pia.
Azam FC ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza mabao 2-0 yaliyotiwa kimiani na Gaudence Mwaikimba dakika ya tisa na Himid Mao dakika ya 36, wote wakimalizia kona za Erasto Nyoni.

Ruvu Shooting walipata pigo dakika ya 32 baada ya kipa wao wa kwanza, Abdul Seif kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo baada ya kugongana na John Bocco wa Azam, hivyo nafasi yake kuchukuliwa na Abdallah Rashid.
Kipindi cha pili, Azam ilirudi kwa kujiamini zaidi na kufanikiwa kupata bao la tatu dakika ya kwanza tu ya kipindi hicho, mfungaji Kipre Herman Tchetche akimalizia pasi pacha wake, Kipre Michael Balou.
Baada ya hapo, Ruvu wakaamua kucheza mchezo wa kujihami kuhofia mabao zaidi.
Mechi hiyo ilikuwa ifanyike jana kwenye Uwanja huo, lakini ikasogezwa mbele hadi leo sababu ya mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha Uwanja ujae maji.
Azam sasa itahitaji pointi tatu zaidi katika michezo yake miwili ya mwisho ili kutawazwa rasmi mabingwa wapya wa msimu wa mwaka 2014/ 2015.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment


Top