Klabu ya Everton imeendeleza wimbi lake la ushindi baada yakufanikiwa kuondoka na pointi zote tatu mbele ya Arsenal. Wenyeji wakianza kwa kasi walianza mchezo kwa kasi na kufanikiwa kujipatia goli la kuongoza kupitia Smith dakika ya 14 kabla ya Lukaku kuandika la pili dakika ya 34, hadi timu zinaenda mapumziko Everton walikuwa mbele kwa goli 2-0.
Kipindi cha pili kilianza na Everton kufanikiwa kutawala mchezo kwa asilimia kubwa, makosa yaliyofanywa na Sagna yaliigharimu timu yake baada yakunyang`anywa mpira na kupelekea wapinzani kugongeana hadi eneo la hatari na kupelekea Arteta kujifunga dakika ya 61. Kwa matokeo hayo ni kama wamelipiza kisasi cha FA mwezi uliopita baada yakuchapwa goli 4-1.
No comments: