Meneja wa Kampuni ya New Position Co.Ltd, Juma Burah akizungumza jambo na waandishi wa habari ofisini kwake.
Meneja akionesha tangazo la kuthibitishwa kwa kampuni yake na Wizara ya Kazi na Ajira katika gazeti la Mtanzania
Meneja aikionesha moja ya mashine ambazo wanahitaji vijana wenye fani ya Mauzo kwa ajili ya kuuza na kusambaza kwa wafanyabiashara.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwajibika kazini.
New Position Co Ltd, ni kampuni iliyosajiliwa kisheria chini ya Wizara ya Kazi na Ajira kwa namba 105407 yenye lengo la kuwaunganisha waajiri na waajiri popote nchini Tanzania.
Kampuni hiyo ni wakala wa ajira na kazi ambayo kazi yake ni kuwatafutia ajira wahitimu wa ngazi mbali mbali wanaohangaika kuomba kazi katika mashirika mbali mbali ikiwa ni pamoja na mashirika au makampuni yanayohitaji wafanyakazi.
Akizungumza na mtandao huu, Meneja wa Kampuni hiyo, Juma Burah amesema watanzania wengi hawajui jinsi ya kuandika barua za kuomba kazi pamoja na wasifu wao(CV) jambo lililopelekea kuanzisha kampuni kwa lengo la kuwakomboa vijana.
Amesema mwombaji wa kazi anapaswa kupeleka vyeti vyake na shilingi elfu kumi na tano(15,000/=)ambazo zitasaidia kupewa mafunzo jinsi ya kuandika cv, barua ya maombi pamoja na kujieleza wakati wa usaili ili muombaji aweze kumudu ushindani uliopo.
Ameongeza kuwa kazi ya kampuni mbali na kutafuta ajira na kazi pia inaibua fursa za ajira kupitia mtandao ambapo sifa za muombaji huwekwa mtandaoni ili wenye kuhitaji wafanyakazi huwapata kiurahisi.
Meneja huyo ameongeza kuwa tangu kusajiliwa kwa kampuni hiyo imepita miezi sita lakini wamepata mafanikio makubwa kwa kuwawezesha wafanyakazi zaidi ya 300 kupata mafunzo na kuajiriwa katika sekta mbali mbali.
Ameongeza kuwa mbali na kampuni kuwatafutia kazi watu mbali mbali pia Kampuni yenyewe inanafasi 50 za wataalamu wa fani ya IT, Mauzo na mapokezi.
Kampuni hiyo pia inaubia na kampuni ya BOLSTO inayohusika na uuzaji wa mashine mbali mbali za Kielectroniki kama vile EFDs ambazo ziko za aina tofauti tofauti ambazo ni Prima, Dp25, Best LC, Ultima na Easy Machines inayofanya kazi ya uwakala wa fedha kama Mpesa, Tigo Pesa, Zuku, Dstv nk.
Amesema pia kampuni hiyo inanafasi 20 za kazi kwa ajili ya kuuza na kusambaza mashine hizo ambapo muuzaji atanufaika na Kamisheni kutokana na mauzo ya mashine hizo
Kampuni hiyo inapatikana katika Jengo la Crdb Ghorofa ya kwanza kushoto au unaweza kupiga simu namba 0718 470499 au kwa barua pepe info@newposition.com au tembelea wavuti wao wa www.new-positions.com. Mbeya mjini.
No comments: