| ||||
Kamanda wa Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani DCP Mohammed Mpinga akiongea na waandishi wa Habari(Hawapo pichani) mikakati ya kupunguza ajali za Barabarani ikiwemo kuongeza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na kuendelea kununua vifaa vya kisasa vitakavyosaidia kupunguza tatizo la ajali nchini,wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. |
Kamanda
wa Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani DCP Mohammed Mpinga
akiwaonyesha waandishi wa Habari(Hawapo pichani) kitabu cha mwongozo cha
askari kwa usalama barabara juu ya yale wanayopaswa kufanya na yale
wanayokatazwa wawapo kazini, wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini
Dar es Salaam.
|
Baadhi
ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano mkutano wa kikosi cha
usalama barabarani, wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es
Salaam. Picha na Hassan Silayo
Na Frank Mvungi
|
Serikali yajipanga kuondoa ajali za barabarani hapa nchini kwa kushirikiana na wananchi.
Hayo
yamesemwa na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Mohamed
Mpinga wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es
salaam.
Akieleza
kamanda Mpinga amesema kwa sasa kikosi cha usalama barabarani
kinashirikiana na vituo vya redio vipatavyo 70 vilivyopo takribani
katika mikoa yote hapa nchini.
Akifafanua
alisema kikosi chake kimekuwa kikiendesha vipindi vya Televisheni na
pia kuendelea kutoa elimu mashuleni ili kuwajengea wananchi uelewa
kuhusu sheria za barabarani.
Kamanda
Mpinga alisema mchakato wa kuanza kuweka nukta kwenye leseni (point
system) kwa madereva watakaovunja sheria za usalama barabarani upo
katika hatua za mwisho na tayari umeridhiwa na Wizara ya Katiba na
Sheria.
Pia
Kikosi cha Usalama barabarani kimeongeza matumizi ya Tehama kudhibiti
ulevi na mwendokasi ikiwa ni sambamba na kuhifadhi takwimu za matukio ya
uvunjaji wa sheria kwa njia ya kielektroniki.alisema Kamanda Mpinga.
Kamanda
Mpinga alisema Kikosi chake kimekwishatoa mwongozo wa utendaji
utakaotumika na askari wa Kikosi cha usalama barabarani ukiwa na lengo
la kuweka kiwango cha utendaji kinachofanana na chenye tija.
Kamanda
mpinga alibainisha kuwa Kikosi chake kimekuwa kikitoa elimu kwa
madereva wa Bodaboda kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama vile chuo
cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) ambapo waendesha bodaboda 4000
wameshapatiwa mafunzo.
Katika
hatua nyingine Kamanda Mpinga amesema Kikosi chake kimekuwa kikifanya
utambuzi wa maeneo hatarishi (Black spot areas) kwa kutumia takwimu za
matukio ya ajali za barabarani.
Kikosi
cha usalama barabarani kimeboresha taratibu za ukaguzi wa magari kwenye
barabara kuu ili kudhibiti madereva wasiozingatia sheria na kanuni za
usalama barabarani.
No comments: