Ilipoishia
Maria alitoa mfuko uliokuwa na chips kuku akampa Johnson akamuambia asihangaike kupika. Johnson alifurahi sana akamtania Maria akamwambia "sijui kama siku nikiwa jela utaniletea vitu kama hivyo"
Maria alitoa mfuko uliokuwa na chips kuku akampa Johnson akamuambia asihangaike kupika. Johnson alifurahi sana akamtania Maria akamwambia "sijui kama siku nikiwa jela utaniletea vitu kama hivyo"
Endelea
Maria: usiseme hivyo mpenzi wangu nani ambaye atakupeleka jela sasa? Johnson: kwani wewe umesahau wazazi wako walisema siku wakigundua kuwa mimi na wewe bado tuna mahusiano watanifunga au watanipoteza duniani?
Maria:
"usiogope mpenzi wangu vile vitisho tu mimi siwezi kukuacha hata wazazi
wangu wafanye nini na siku wakikufanyia kitu kibaya tu basi mimi watanikosa
naweza nikajiua kwa ajili yako"
Johnson: "hayo maneno unaongea
kwa vile tu tupo wote hapa siku mimi nikifa au nikifungwa utanisahau tu na
utapata mwanaume mwingine sababu wazazi wako hawataki uwe na mtu kapuku kama
mimi wanataka wakusomeshe uje uolewe na mtu mwenye pesa siyo mimi muuza
genge"
Machozi yalianza kumtoka Maria alivyosikia yale
maneno ya Johnson akamwambia "Johnson baby usiongee maneno kama hayo mimi
nakupenda wewe na hiyo hiyo hali yako uliyonayo na ukumbuke tumetoka mbali sana
kwa hiyo mimi siwezi kukuacha hata iwaje"
Johnson: "haya mpenzi si tupo
tutaona tu mwisho wake utakuwaje tumuombe tu Mungu atusaidie"
Johnson na Maria waliongea mengi sana hadi muda wa
kulala ulivyofika wakalala zao.
Saa 12 asubuhi kama kawaida Johson aliamka akaanza
kujiandaa kwa ajili ya kuwahi gengeni kwake akamuamsha na Maria. Mpenzi amka ujiandae uwahi kwenu kumbuka leo wazazi wako ndio
wanarudi safari wasije wakakukosa wakatuletea balaa.
Maria: "baby wewe wahi tu mimi
niache nipumzike kidogo nitaamka saa nne ndo nitaenda nyumbani siwezi kuwahi
asubuhi yote hii"
Johnson: "siwezi kuondoka na
kukuacha wewe hapa kwangu nitakuwa sina amani nitakaa kwa wasiwasi we amka
ujiandae utaenda kupumzika hata kwenu"
Johnson na Maria walibishana sana lakini mwisho
Maria alikubaliana na mpenzi wake akamka akajiandaa wakatoka wote pamoja wakawa
wanaelekea kwenye kituo cha daladala.
Wakati wapo njiani wanapiga stori zao Johnson
akakumbuka yale maneno ya mzee Joseph aliyomuambia kuwa akimtumia vizuri Maria
anaweza akamtoa kimaisha.
Johnson: "Mpenzi nimekumbuka
kitu yule mzee wa kule gengeni kwangu jana aliniambia anataka kuongea na sisi
kwa hiyo ukipata muda uje kule gengeni kwangu tumsikilize anasemaje"
Maria: "sawa mpenzi wangu lazima
nikipata muda nije yule mzee tangu siku ile atupatanishe na kutuambia yale
maneno nimetokea kumpenda sana na kumuheshimu."
Maria hakujua kuwa Johnson alitaka kumpambanisha
kwa yule mzee ili ampange aanza kumpa pesa za kuendeshea biashara zake, wakati Johnson na Maria wapo kwenye kituo cha
daladala wanaendelea kuongea simu ya Maria ikaita kucheki alikuwa ni mama yake
Maria alistuka sana akajua tayari wazazi wake tayari wameshafika nyumbani kwao ndio maana wanampigia simu. Alipokea ile simu wakasalimiana na mama yake mama
yake akamwambia "mwanangu Maria mwambie housegirl atuandalie chakula
kizuri tupo njiani tunarudi tuna njaa sana"
Maria: "sawa mama
namwambia mtakuta tumewaandalia chakula kizuri." Wazazi wa Maria hawakujua
kuwa muda huo wanapiga simu Maria yupo na Johnson walijua kalala nyumbani
Johnson alichanganyikiwa Maria alivyomwambia zile
habari kuhusu ile simu aliyopigiwa, hakutaka kupoteza muda akaita bodaboda Maria
akapanda akaondoka zake, Johnson akapanda daladala safari ya kwenda gengeni
kwake ikaanza huku akimuomba Mungu Maria afike haraka nyumbani kwao kabla wazazi
wake hawajafika.
Itaendelea............
Itaendelea............
No comments: