Ilipoishia
Maria alipanda boda boda akaanza safari ya kwenda kwao
Jonhson na yeye akapanda daladala akaanza safari ya kwenda gengeni kwake huku
akimuomba mungu Maria awahi kufika kwao kabla wazazi wake hawajafika
Endelea Johnson alifika gengeni kwake akafungua akafanya usafi akaanza kupanga bidhaa zake. Alivyomaliza akatoa simu yake akampigia Maria ili ajue kinachoendelea huko nyumbani kwao Maria alivyopokea simu Johnson akamuuliza "vipi mpenzi wangu umefika salama nini kinaendelea huko?
Maria: "nashukuru Mungu nimefika salama mpenzi na
nimewawahi baba na mama ila housegirl kaniambia jana usiku walimpigia simu
wakamuuliza kama mimi nipo nyumbani akawajibu ndiyo nipo, Mama akamuambia anipe
simu niongee naye housegirl akawadanganya nimelala nimekataa kufungua mlango wa
chumbani kwangu"
Johnson: "Si unaona sasa mimi toka jana
nimekuambia wazazi wako bado wana wasiwasi na wewe mshukuru sana huyo housegirl
wenu kakusaidia sana asingetumia huo ujanja sijui ingekuwaje"
Maria:
"huyu housegirl wetu mtoto wa mjini ndio maana nampenda hata mlinzi
wetu pia mjanja mpenzi kwa hiyo wala usiogope hakiharibiki kitu"
Johnson:
"poa mpenzi fanya kama nilivyokuambia ukipata muda mzuri uje huku gengeni
kwangu umsikilize mzee Joseph anataka kukuambia nini"
Johnson alimaliza kuongea na Maria akakata simu, muda
huo huo akamfuata mzee Joseph kwenye kiduka chake. Wakasalimiana pale wakataniana kidogo kama kawaida yao
mzee Joseph akamtania Johnson akamwambia "we kijana safari hii lazima
nikuibie yule mtoto yani wewe una msichana kwao wana mapesa vile halafu hadi
leo unauza hicho kigenge chako ngoja wajanja tumuibe uone tunavyomtumia
vizuri"
Johnson alicheka sana kusikia yale maneno ya mzee
Joseph akamwambia "we mzee ushazeeka sasa hivi hayo mambo tuachie vijana
kwanza huwezi kumuiba yule mtoto hapa amefika hasikii wala haoni mimi namkuna
vizuri ndio maana kadata sasa wewe mzee utampa raha gani mtoto mbichi kama
yule"
Mzee Joseph: "we kijana ng'ombe hazeeki maini mimi
nikimchukua yule kwako harudi tena anakusahau'’
Mzee Joseph na Johnson walitaniana pale wakacheka
sana Johnson akaanza kumuelezea yule mzee kilichompeleka pale. Akamuambia Mzee yule msichana wangu jana kaja kulala
kwangu leo asubuhi wakati namsindikiza nikakumbuka yale maneno uliyoniambia
siku ile kuwa nimjaribu nimuombe aniongezee mtaji mimi nimeogopa kumuambia hilo
swala kwa hiyo nimemwambia akipata muda aje hapa gengeni kwangu ili niongee
naye hilo swala wakati na wewe upo unisaidie kumpa maneno hadi aelewe. Mzee Joseph alimsikiliza Johnson kwa makini akamuambia
"we kijana muoga sana unamuogopa hadi mpenzi wako wakati kila siku
mnavuliana nguo haina shida ngoja aje tujaribu kumpanga kama ataelewa ila
mchongo ukiwa poa lazima unipe na mimi mzee wako pesa ya pombe"
Johnson akacheka akamwambia "usijali mzee mimi
na wewe tena nakukubali sana mzee wangu"
Wakati Johnson anaongea na mzee Joseph simu yake
ikawa inaita kucheki alikuwa ni Maria akapokea lakini akashangaa kumsikia Maria
analia kwenye simu
Itaendelea………………………..
Itaendelea………………………..
No comments: