Kaimu
Meneja Sehemu ya Habari toka Wakala wa Vipimo Bi. Irene John akiwaeleza
jambo waandishi wa Habari (hawapo pichani) na kuwatahadharisha wananchi
kuhusu matumizi ya vipimo batili unaofanywa kwa kusutumia visado na
ndoo za Plastiki. Wanaofuata Kushoto kwake ni Afisa Habari Idara ya
Habari (MAELEZO) Frank Mvungi,Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi Bw. Peter
Masinga na Mwisho ni Meneja wa Upimaji Bw. Richard Kadeghe.
Mkuu
wa Kitengo cha Sheria Toka Wakala wa Vipimo Bw. Moses Mbunda akiwaeleza
waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mchakato wa Kunazisha
Sheria Mpya itakayosaidia kuimarisha Sekta ya Upimaji Nchini, Kulia ni
Kaimu Meneja Sehemu ya Habari toka Wakala wa Vipimo Bi. Irene John.
Meneje
wa Upimaji toka Wakala wa Vipimo Bw. Richard Kadeghe akiwaonyesha
waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi ambavyo vipimo batili
vinayotumika.
Baadhi
ya waandishi wa Habari waliohudhuria mkutano wa Wakala wa Vipimo leo
Jijini Dar es Salaam.
Na Frank Mvungi MAELEZO
Serikali yawatahadharisha wananchi kuhusu matumizi ya vipimo batili hususani visado na ndoo za Plastiki.
Hayo yamesema na Kaimu Meneja wa Habari,Elimu na Mawasiliano wa EWakala wa Vipimo Tanzania Bi Irene John wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Akieleza Bi Irene amesema ufungashaji na upimaji batili ni kinyume cha sheria ya Vipimo sura 340 (iliyopitiwa mwaka 2002) pamoja na Kanuni zake.
Akifafanua zaidi alisema ufungashaji na matumizi ya vipimo batili hudhoofisha uchumi wa Taifa kwa kuwa humpunja mkulima,mlaji,mfanyabiashara na mtumiaji.
Aliongeza kuwa Serikali imekuwa ikipoteza mapato yake ambapo Halmashauri hukusanya mapato pungufu wanapotoza ada kwa gunia badala ya uzito au ujazo.
Arene alitaja athari nyingine kuwa ni kuathiriwa kwa biashara ya kimataifa kutokana na wananchi kutokuzingatia vipimo hasa kwa kutumia mizani wakati wanapofanya biashara ya kununua na kuuza.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya ufundi wa wakala huo bw.Peter Masinga alisema ni vyema wananchi wakaacha kutumia vipimo batili kwani vimekuwa vikidhoofisha ukuaji wa uchumi kwa muda mrefu na hivyo kwenda kinyume na jitihada za Serikali za kuwaletea maendeleo wananchi.
Bw. Peter aliongeza kuwa kuanzishwa kwa vituo vya kununulia mazao vijijini ni moja ya hatua zitakazosaidia kuondoa tatizo la vipimo batili kwa kuwa Serikali itaweza kusimamia kwa ukaribu matumizi ya vipimo sahihi kama vile mizani.
Wakala wa vipimo ni Wakala wa Serikali ambayo ilianzishwa Mei,2002 kwa Tangazo la Serikali namba 194 kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma bora kwa wananchi, jukumu kuu likiwa kumlinda mtumiaji kupitia matumizi ya vipimo sahihi.
No comments: