ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5

Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akifungua mafunzo ya Ukimwi mahali pa kazi kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa mwishoni mwa juma, Semina hiyo iliyoandaliwa na idara ya maendeleo ya jamii na mratibu wa TACAIDS Mkoa wa Rukwa kwa watumishi hao ilikua na lengo la kuelimishana na kukumbushana juu ya mambo mbalimbali yanayohusu janga la Ukimwi na umuhimu wa Tohara kwa wanaume katika kujikinga na janga hilo. Katika hotuba yake Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa hakusita kuonyesha hisia zake kali kwa watumishi watakaohusika katika rushwa za ngono na kusema kuwa watachukuliwa hatua kali bila ya utetezi wowote kutoka kwake.
Mratibu wa TACAIDS Mkoa wa Rukwa Ndugu Daniel Mwaiteleke akitoa mada juu ya uelewa wa jumla kuhusu gonjwa la UKIMWI kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa katika mafunzo ya siku moja yaliyofanyika katika ukumbi wa RDC Mjini Sumbawanga.
Muwezeshaji wa mada ya magonjwa ya zinaa STD na STI Dkt. Lunyelele akiwasilisha mada yake kwa umahiri mkubwa bila ya kutafunatafuna maneno.
Dkt. Lunyelele akiwa anatoa mafunzo hayo.
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mafunzo hayo.
Mjumbe katika Semina hiyo Ndugu Frank Mateny akichangia moja ya mada katika mafunzo hayo.


 

                   Picha na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment


Top