Bayport yazindua Bima Ya Elimu,Kwenye hafla ndogo kwenye ofisi ya Wizara ya Maendeleo
ya Jamii, Jinsia na Watoto. Kuanzia mkono wa kushoto katika picha ni
Mhe. Sophia Simba (Waziri) akifutiwa na wawakilishi wa Bayport Financial
Services Maneja Masoko Ngula Cheyo na Matthew Mbaga, Meneja wa Bima.
Bayport Financial Services, ambayo ni moja kati ya
wakopeshaji akubwa kwa ajili ya wafanyakazi imezindua mpango wa bima kwa ajili
ya elimu.
Mfumo huo wa bima ni kwa ajili ya
kuendeleza elimu kwa watoto pale ambapo wazazi wao wanafariki. Kwa kiwango cha
chini cha TZS 2,500 kwa mwezi, bima hii ni nafuu kwa wafanyakazi wenye kipato
cha chini na inamhakikishia mwanafunzi kupata mahitaji yake ya msingi katika
elimu.
Akiongea katika
ufunguzi wa huduma hii mpya jana, Meneja Masoko wa Bayport Financial Services,
Ngula Cheyo aliwaeleza waandishi wa habari kwamba lengo la kubuni huduma hii ni
kutokana na kuwepo kwa pengo kwenye soko la huduma ambayo inakidhi watu wenye
kipato kidogo. ‘Kuwepo kwetu hapa Tanzania kwa muda mrefu kumetupa fursa ya
kutambua kuwa huduma ya bima haiwafikii watu wengi na huduma hii ingewanufaisha
watanzania wengi ambao wanajali watoto wao’, alisema Ngula.
Katika uzinduzi huo uliofanyika
ofisini kwake, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, jinsia na Watoto, Meshimiwa Sophia
Simba, aliisifu kampuni ya Bayport Financial Services kwa kuzindua huduma hii
ambayo itasaidia kupunguza mzigo kwa ndugu wa mfiwa na kuhakikisha motto
anaendelea na elimu yake. ‘Elimu ni haki ya kila mtoto na huduma hii itapunguza
wanafunzi ambao wanaacha shule kwa sababu ya kushindwa kulipa ada pindi wazazi
au walezi wao kufariki. Elimu inasaidia watanzania wengi kujikomoa na umasikini
na kusiwe na pingamizi yoyote kwa mtoto kutoipata,’ alisema Mheshimiwa Simba.
Wazazi na walezi
wanauwezo wakuchagua jinsi ya kulipa na idadi ya wanafunzi wanaotaka kuwalipia
bima hii. Bima hii inapatikana katika matawi yote ya Bayport ambayo yamesambaa
katika mikoa yote hapa nchini. Matthew Mbaga ambaye ni Meneja wa Bima pia
alieleza waandishi pia umuhimu na manufaa ya bima hii katika uzinduzi huo.
No comments: