Ubaguzi
wa rangi umezidi Hispania, baada ya mchezaji wa Levante, Pape Diop
kuzomewa na kufanyiwa ishara za nyani jana na mashabiki wa Atletico
Madrid wakati wa mechi ya La Liga.
Wiki moja
baada ya beki wa Barcelona, Dani Alves alipolazimika kula ndizi
aliyotupiwa na mashabiki, kiungo huyo wa Senegal alisema alicheza kama
nyani mbele ya waliomzomea na kumkebehi.
"Waliniita
nyani,niligeukia na kujifanya nyani," alisema Diop na kukaririwa na
Marca.com. "Nimechoka na ubaguzi katika soka. Na upo mwingi.
Wachezaji wa Atletico, Diego Godin na Diego Costa wakimfuata Diop anayeshangilia kwa kucheza kama nyani
"Nilicheza
kama nyani kuliainisha tatizo. Nilitaka watu wajue kilichotokea. Sijui
kama ni ubaguzi, au kudharauliana, lakini wanatakiwa kuacha ishara za
nyani wanazowafanyia watu,"alisema.'
Alves
alipata sapoti kubwa kutoka kwa wachezaji wake na Rais wa FIFA, Sepp
Blatter baada ya tukio lilitokea katika mechi na Villarreal wiki
iliyopita.
Mashabiki
wa Atletico jana waliondoka wanyonge baada ya bao la kujifunga la
Filipe Luis na lingine la David Barral kuopunguza matumaini yao ya
kutwaa ubingwa wa La Liga baadaye mwezi huu
Diop (kulia) akiteleza miguuni mwa Toby Alderweireld wa Atletico kuondosha mpira jana Levante ikishinda 2-0
Wachezaji wa Atletico kutoka kushoto Filipe Luis, Thibaut Courtois na Adrian Lopez wakiondoka kinyinge baada ya mechi jana
No comments: