Sultani na mtawala wa Brunei ambaye ni mmoja wa matajiri wakubwa duniani. |
Serikali ya Brunei iliyo Kusini Mashariki mwa Bara Asia, itaanza kutumia sheria kali za kiisilamu.
Kiongozi wa nchi hiyo ya kiisilamu ambayo ni jirani na Malaysia ametangaza kuwa sheria hiyo itaanza kutumika kuanzia wiki hii.
Adhabu
zilizo chini ya sheria za kiisilamu ni pamoja na kuwakata wezi mikono
na kuwapiga mawe hadi kufa watu waliopatikana na hatia ya kushiriki
Zinaa.Sheria hii itatekelzwa katika awamu tatu katika kipindi cha miaka mitatu.
Umoja wa Mataifa tayari umeelezea wasiwasi wake kuhusu sheria hiyo.Taifa
la Brunei tayari linafuata sheria kali za kiisilamu kuliko hata nchi
jirani kama Malaysia na Indonesia pamoja na kuharamisha uuzaji na
utumiaji wa pombe.
Nchi
hiyo ndogo ilio katika kisiwa cha Borneo,inatawaliwa na Sultan Hassanal
Bolkiah na imepata utajiri wake kutokana na kuuza nje mafuta na gesi
yake.
Takriban nusu ya waisilamu wanaoishi katika nchi hiyo ni raia wa Malaysia.
Sultani
alinukuliwa akitangaza hatua ya kwanza ya kuanza kutumiwa kwa sheria
hiyo akimshukuru Mungu na kuwatahadharisha wananchi kuhusu kuanza
kutumika kwa sheria hiyo.
Sheria
yenyewe itaanza kutumika katika kipindi cha miaka mitatu huku hukumu ya
makosa ya kwanza ikiwa kifungo cha jela pamoja na kutozwa faini.
Katika
awamu ya pili ndipo wahalifu wataanza kukatwa mikono kwa
watakaopatikana na hatia ya wizi , huku awamu ya tatu ikihusu kupigwa
mawe wazinifu na wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Sultani
anayetawala kisiwa hicho ni mmoja wa matajiri wakubwa duniani na tayari
amewaonya watu kukoma kushambulia mipango yake kupitia mitandao ya
kijamii.
Mfumo wa sheria katika mahakama nchini humo ni sawa na ule wa Uingereza.
Umoja
wa Mataifa uliitaka serikali kuchelewesha mageuzi hayo ili kuhakikisha
kuwa sheria hiyo inaambatana na sheria za kimataifa kuhusu haki za
binadamu.
Credits: BBC
No comments: