Mbunge
wa Jimbo la Kigamboni,Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akizungumza
jambo wakati wa hafla ya kupokea Vifaa vya Solar kutoka kampuni ya Steps
Solar kwa ajili ya Kituo cha Polisi cha Polisi cha Mjimwema,Kulia ni
Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps Solar,Dilesh Solank.
Mmoja wa Mabalozi wa Steps Solar,Jacob Stephen akiongea na wananchi wa Mjimwema.
Mabalozi wa Steps Solar Jacob Stephen (JB) na Amri Athuman (King Majuto) wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mwigizaji
mkongwe katika tasnia ya filamu nchini,Amri Athuman ‘King Majuto’ wiki
iliyopita akiwa kama Balozi wa Steps Solar alitoa msaada wa kukifungukia
Solar kituo cha Polisi cha Mjimwema, ikiwa ni katika kampeni za
kuhakikisha kila mtanzania anafaidika na matumizi ya nishati ya umeme
Nuru.
Akiongea
na Waandishi wa habari katika hafla iliyoandaliwa na kampuni ya Steps
Entertainment ambao ndio wafadhali wa msanii huyo, alisema kuwa kampuni
hiyo imekuwa ikisambaza filamu zake lakini kuna utaratibu wa kutoa
misaada kwa jamii, kwake yeye ameona tatizo linalowakabili watu wengi
nje ya miji ni umeme.
“Nimeanza
kampeni kama Balozi wa Steps Solar kuwasaidia wapenzi wa kazi zangu,
ambazo ninaamini bila wao siwezi kabisa kuwa King, kama vile mnavyopenda
kuniita, nimeanza katika kituo cha Polisi cha Mjimwema lakini nikiwa na
wenzangu tutafika sehemu nyingi zaidi,”alisema King Majuto.
Afisa
mahusiano wa kampuni hiyo Moses Mwanyilu amesema kuwa mradi huo ni
endelevu ambapo wanatarajia kufunga Steps Solar katika Kituo cha Yatima
Tuangoma, Mjimwema, vituo vya Polisi ni Mjimwema na Ferry, vituo vya
afya ni Mjimwema, Ungindoni, Homboza Chanika na Tuangoma.
Msanii
huyo aliambatana na wasanii wengine ambao pia ni mabalozi wa Steps
Solar, ambao ni Jacob Stephen ‘JB’ na Salma Jabu ‘Nisha’ mgeni wa
heshima katika hafla hizo alikuwa Mh. Dr. Faustine Ndugulile mbunge wa
Kigamboni.
No comments: