Mkuu wa wilaya ya Ulanga akiwa katika moja ya Boti kivukoni siku ya mei mosi katika ziara. ya kukagua hali ya huduma kivukoni. |
Wito
umetolewa kwa wamiliki wa boat ndogo katika maeneo mbali mbali kuzileta
katika mto kilombero ilikutoa huduma ya usafiri kwa wakazi wa Kilombero
na Ulanga kutokana na maji kuendelea kuongezeka katika mto Kilombero.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Ulanga MH, Francesi Miti wakati akizungumza na wananchi wa kivukoni na wasafiri jana katika eneo la kivuko alipofika kuangalia hali ya huduma za usafiri katika mto Kilombero.
Mitti amewataka wasafiri
wote wanaotumia usafiri wa boat zilizopo sasa ambazo ni boti ya sakosi,
boti ya halmashauri ya wilaya ya ulanga, boat ya sua, kuvaa maboya
ilikuweza kuwa salama zaidi wanapo kuwa katika vyombo hivyo vya usafiri.
Mapema
Miti akiwa katika eneo hilo wananchi na wasafiri walilalamikia bei ya
boat hizo ambapo mtu mmoja alikuwa akivushwa kwa shilingi 2000 kutoka
bei ya kawaida ya shilingi 200 kwa pantoni ya kivuko,ambapo baada ya
mazungumzo na wasafirishaji bei imeshuka hadi kufikia shilingi 1500 kwa
mtu mmoja, huku mitumbwi ikipigwa marufuku kutoa huduma ya usafiri
kutokana na kasi ya maji katika mto kilombero.
Miti
aliambatana na kamati ya Ulinzi na usalama wilaya, kaimu mkurugenzi wa
wilaya ya ulanga, mwenyekiti wa chama cha ccm wilaya ya ulanga, viongozi
mbalimbali wa serikali na wajumbe wengine wa chama.
No comments: