Ilipoishia
Wakati Johnson anaongea na Mzee Joseph akasikia simu
yake inaita kucheki alikuwa ni mpenzi wake Maria alipokea ile simu alishangaa
kusikia Maria analia
Endelea
Johnson hakuelewa Maria analia nini akabaki anashangaa tu akajua mambo yameshaharibika huko kwao. Akamuuliza "vipi mpenzi mbona unalia nini kimetokea?? Maria akamjibu "yani mpenzi we acha tu hapa nilipo mimi nimechanganyikiwa Baba na Mama wamerudi na habari mpya eti wameniambia wamenitafutia shule Uganda wanataka nikasome kule" Johnson akamwambia "sasa ndio ulie mpenzi mimi nilijua kuna kitu kimetokea kumbe shule we wasikilize wazazi wako wanapenda binti yao usome baadae uwe na maisha mazuri kama wao kama wamekutafutia huko we nenda tu mpenzi" Maria akamuambia Johnson "mpenzi hata wafanyaje mimi Uganda siendi mimi nishakuzoea mpenzi wangu mimi nimeshazoea kuwa karibu na wewe Uganda nikafanye nini hata nikienda huko sitasoma kabisa zaidi ya kuumwa hovyo na kukonda sababu ya kukuwaza wewe" Johnson akamuambia "mimi nipo tu mpenzi ukienda ukirudi utanikuta tumuombe tu Mungu na wazazi wako wameshaamua huwezi kuwapinga na wakijua kuwa unagoma kwenda kwa sababu yangu utaniingiza tena kwenye matatizo" Maria akamwambia "Mpenzi baadae nakuja gengeni kwako tuongee vizuri ila mimi msimamo wangu ndio huo siendi hata kwa dawa huko Uganda" Johnson akamuuliza Maria "Baadae utakuja vipi wakati wazazi wako wamesharudi? Akamjibu "nimewasikia wanaongea hapa kuwa baadae watatoka wakitoka tu na mimi natoka nakuja huko gengeni kwako" Johnson alivyomaliza kuongea na Maria akaguna huku anatingisha kichwa Mzee Joseph akamuuliza "vipi tena kijana wangu kuni nini?
Johnson: "naona mpango wetu wa kuanza kuchukua
pesa kwa Maria unabuma"
Mzee: "kwanini unasema hivyo?
Johnson akamsimulia mzee Joseph
inshu nzima kama alivyoambiwa na Maria
Mzee: "usiogope kijana kama kweli yule binti
anakupenda hawezi kukubali kwenda huko Uganda na wazazi wake hawawezi
kumlazimisha kama yeye hataki"
Johnson: "lakini Mzee we huoni kwamba wazazi wake
wakija kujua mimi ndio nimesababisha mtoto wao agome kwenda kusoma huko uganda
itakuwa majanga kwangu"
Mzee: "acha uoga kijana watajuaje wewe ngoja
yule binti aje hapa leo tuongee naye tusikie anasemaje ndio tutajua cha
kufanya"
Johnson aliongea mambo mengi sana na Mzee Joseph
walivyomaliza maongezi yao akaenda zake gengeni kwake. Alikuwa anamsubiria Maria kwa hamu sana aone Mzee Joseph
jinsi atakavyompanga alitoa simu yake akampigia Maria akamuuliza yuko wapi
Maria akamuambia yupo njiani anakuja gengeni kwake Johnson alifurahi sana
kusikia vile muda huo huo akamfuata Mzee Joseph akamuambia ajiandae Maria yupo
Njiani anakuja. Hawakukaa hata sana Maria
akafika pale gengeni kwa Johnson akamfuata hadi pale walipokaa na mzee Joseph
akawasalimia wote wawili na yeye akakaa. Johnson
akawa anamuangalia mzee Joseph aone ni jinsi gani atakavyomuingia Maria kuhusu
lile swala lake.
Mzee Joseph: "binti umependez sana kweli Johnson
anajua kuchagua "
Maria akacheka kusikia vile
Itaendelea...................
Itaendelea...................
No comments: