ads

Slider[Style1]

Style2

Style3[OneLeft]

Style3[OneRight]

Style4

Style5



 Ilipoishia
Johnson alimshika Maria kiuno wakaongozana hadi bajaji zinapopaki Maria akapanda akaondoka zake
Endelea
Maria alivyoondoka Johnson alimfwata tena mzee Joseph, mzee nimekukubali sana yani umempanga mtoto na maneno matamu hadi ameelewa.
Mzee Joseph: "mimi nimezeeka ila nina maujanja kibao sasa wewe kijana damu bado changa unazubaa unakuwa muoga wakati yule mtoto yupo vizuri nyumbani kwao pesa ipo na anakupenda kweli."
Johnson: "kweli mzee hapo tayari umenifungua ngoja nianze kula pesa za mpenzi wangu mimi nilikua namuonea aibu nilikua naogopa sana kumuambia shida zangu."
Mzee Joseph: "huo uoga wako ndio ungekufanya uendelee kuteseka ungeuza genge hapa hadi uzeeke, sasa hivi wewe tulia muheshimu mpenzi wako muonyeshe mapenzi ya ukweli atakusaidia tu mimi nimemsoma yule binti hana tatizo si unaona hapa hapa tumepewa hela nzuri ya kula."
Johnson akacheka sana kusikia yale maneno ya mzee Joseph akamwambia "kweli mzee tumepata pesa ambayo hata hatukuitegemea, ahsante sana mzee mimi najua bila wewe hata nisingeipata hii Elfu ishirini yani nimekaa na mpenzi wangu miaka yote hiyo naogopa kumuomba pesa kumbe hana tatizo"
Johnson na Mzee Joseph waliongea mengi sana mzee Joseph akamaliza kwa kumuambia Johnson "Ila sasa nyie vijana wa siku hizi mna matatizo sana utakuta hapo binti wa watu atafanya juu chini atakupatia pesa utaanza kufanya biashara kubwa siku tu ukianza kuwa na pesa nyingi ukifanikiwa unaanza kumdharau na kumtesa binti wa watu hapo utaanza ulevi utaanza kuwa na wanawake wengi nakuomba sana kijana wangu usije ukafanya hivyo utaharibu kila kitu dunia ya sasa imeharibika sana."
Johnson: "mimi siwezi kufanya hivyo mzee wangu Maria nimetoka naye mbali sana nampenda sana kwa hiyo hata siku nikija kufanikiwa siwezi kumfanyia mambo ya ajabu wala siwezi kumsaliti."
Mzee Joseph: "sawa kijana wangu itakuwa vizuri sana kama kweli siku ukifanikiwa hautabadilika kama bado nitakuwa hai nitaona tu"
Johnson alimshukuru sana mzee Joseph kwa kumpa somo akamuaga akaenda gengeni kwake alikaa kidogo akaanza kufunga sababu giza lilikuwa limeanza kuingia. Alipomaliza kufunga genge lake akaenda kupanda daladala safari ya kurudi kwake ikaanza huku akiwa na furaha sana kwanza alijipatia Elfu ishirini ya bure ile siku kutoka kwa mpenzi wake kingine kilichomfanya awe na furaha ni vile Maria tu alivyokubali kumuongezea mtaji abadilishe biashara. Alifika kwake akatua mizigo yake akaenda kuoga alivyomaliza akajipikia chakula akala akajilaza kitandani akachukua simu yake akaanza kuchati na Maria, vipi mpenzi wangu ulifika salama? 

Maria: "ndiyo mpenzi nimefika salama ila sina raha kabisa Baba na Mama wanazidi kunichanganya kichwa changu mimi nakataa kwenda kusoma huko Uganda wenyewe wananilazimisha sijui nifanyaje natamani hata kutoroka hapa nyumbani"
Johnson: "sasa mpenzi kwanini utoroke kwenu kwa sababu ya shule wewe wasikilize wazazi wako nenda tu ukasome huko Uganda"
Maria: "mpenzi mimi siwezi kwenda Uganda nitakumisi sana kwanza najua masomo hayatapanda kabisa nitaumwa hovyo, nitakonda bure mimi nimeshakuzoea mpenzi wangu siwezi kukaa mbali na wewe"
Johnson: "mpenzi mimi nimekwambia utanikuta nakusubiri wala usiwe na wasiwasi hivi unazani siku wazazi wako wakigundua unakataa kwenda huko shule kwa sababu yangu unafikiri itakuwaje si utanisababishia matatizo?"
Maria: "wala usiogope mpenzi mimi nitamalizana nao mwenyewe halafu kesho jiandae nitakufuata gengeni kwako tutaongozana kuna vitu nataka nikakununulie"
Johnson alifurahi sana kusikia vile japo hakujua anaenda kununuliwa vitu gani

Itaendelea…………………………..

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment


Top