Ilipoishia
Johnson alimaliza kufunga genge lake akawa anamsubiri Maria aje waondoke
Endelea
Mzee Joseph akamuambia Johnson "sasa kijana mimi ngoja niondoke zangu usisahau kuniletea na mimi zawadi umuambie mpenzi wako mzee Joseph na yeye anataka zawadi ya ukumbusho"
Johnson: "sawa mzee hata usijali lazima nikuletee zawadi yako sababu bila wewe nisingepata maujanja yote haya"
Mzee Joseph akacheka sana akamuaga Johnson akaondoka zake, haukupita muda mrefu sana Johnson akaona bajaji imekuja hadi pale gengeni kwake alikuwa ni Maria hawakutaka kupoteza muda akaingia ndani ya bajaji safari yao ikaanza walisalimiana kwa mabusu mazito wakajuliana hali Johnson akaamua kuuliz, mapenzi tunaelekea wapi niambie basi nijue?
Maria: "nataka twende Mwenge nikakufanyie shopping tukitoka pale tuelekee kwenye duka flani nikakununule baadhi ya vitu vya ndani ambavyo pale kwako huna"
Johnson alifurahi sana kusikia vile hakutegemea kama siku moja Maria atamfanyia mambo makubwa kama yale alikuwa hawazi kabisa hicho kitu. "Nashkuru sana mpenzi wangu utakuwa umenisaidia sana" Maria: "kawaida tu mpenzi wangu nakupenda sana nitakufanyia mambo makubwa sana utafurahi tumuombe mungu"
Johnson: "na vipi safari yako ya kwenda Uganda wazazi wako wanasemaje?
Maria: "Wazazi wangu bado wananikomalia nikasome kule wanasema eti hapa sisomi nina mambo mengi, nina marafiki wengi na bado wanahisi mimi na wewe tuna mahusiano lakini mimi siwezi kukubali nikasome Uganda nikuache wewe mpenzi nimeshakuzoea sana nikienda kule nahisi nitakuwa nakufikiria wewe tu sidhani kama nitasoma"
Johnson: "lakini mpenzi ukiona wazazi wako wamekukomalia sana inabidi tu uwasikilize uende sababu ukikataa unaweza hata mimi ukaniingiza kwenye matatizo sababu umeshasema wanahisi bado tuna mahusiano, ndio maana hautaki kwenda huko Uganda"
Maria: "wewe wala usiogope mpenzi wangu mimi wazazi wangu wananipenda sana wananisikiliza sana nikikataa kitu hawawezi kunilazimisha"
Johnson na Maria waliongea mengi sana mule ndani ya bajaji dereva hata hakuwa na muda nao alikuwa anawasikiliza tu hadi wakafika mwenge Maria akamlipa yule dereva pesa yake wakateremka.
Maria alimpeleka Johnson kwenye duka kubwa la nguo Johnson alikuwa anashangaa tu sababu hakuwahi kuingia kwenye duka kama lile wala hakutegemea kama ipo siku ataenda kufanya shopping kwenye duka kubwa kama lile.
Maria: "mpenzi wangu chagua nguo na viatu unavyovitaka wala usiogope mimi nalipa hapa tumekuja kwa ajili yako"
Johnson akawa anaangalia anaona vitu vyote kwenye lile duka kama ni vya gharama sana Maria alivyoona Johnson kama anaogopa akamuambia "Mpenzi basi ngoja nikuchagulie vitu vikali ambavyo kwa jinsi ulivyo ukivaa lazima upendeze"
Maria alimchagua Johnson viatu moka, raba pamoja na sendrozi nzuri za kisasa akamchagulia suruali za vitambaa na Jeans akamchagulia mashati na tisheti na vitu vingine vidogo vidogo. Johnson alifurahi sana alimshukuru sana Maria sababu hakuwahi kufikiria kama ipo siku atamfanyia mambo kama yale.
Walitoka kwenye lile duka wakaenda sehemu kupata chakula ili aendelee na mambo mengine, walivyomaliza kula wakaelekea kwenye duka la vyombo Maria akamnunulia Johnson baadhi ya vitu ambavyo alikuwa hana pale kwake Johnson alifurahi sana ile siku walivyotoka pale Maria akamuambia "mpenzi kwa leo hivyo vimetosha tukija siku nyingine tutaongeza vingine kwa sasa tuchukue bajaji twende kwako ukaweke hivi vitu"
Johnson hakuwa na neno tena alipanga kumpa penzi la nguvu Maria ile siku sababu alimfurahisha sana
Itaendelea…………………..
Slider[Style1]
Style2
Style3[OneLeft]
Style3[OneRight]
Style4
Style5
Tagged with: SIMULIZI
About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
- Popular Post
- Video
- Category
Películas populares
-
Simulizi kali ya kutisha iliyoandikwa na Amir Malick, imeanza leo sehemu ya kwanza...
-
ILIPOISHIA: “MAMAA.. MAMAAAAAAAAAAAAA….!!!” Kelele zilisikika kutoka ndani ali...
-
ILIPOISHIA: Macho yalikuwa yamebadirika rangi na kuwa myekunduuu kama amemwagiwa maji ya p...
-
MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA III – (NAFASI 100) Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.
-
Ilipoishia Maria alimpigia Johnson simu akamwambia anataka akalale tena nyumbani kwake Johnson akamgomea akamwambia asije sababu waz...
-
COMPUTER SYSTEM ANALYST II (MOBILE APPLICATIONS DEVELOPMENT/PROGRAMMER) POSITION DESCRIPTION: COMPUTER SYSTEM ANALYST II (...
-
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte) limesema kuanzia mwaka huu wa masomo, wanafunzi wanaotaka kujiunga na masomo ngazi ya astasha...
-
Ilipoishia Mzee Joseph akamuambia Maria "Binti umependeza sana we mrembo kweli Johnson anajua kuchagua" Maria akacheka kusikia...
-
The Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) is focusing on increasing the outreach and service quality of its Energy products f...
-
Ilipoishia Johnson alipanga kumpa Maria penzi zito ile siku sababu alimfurahisha sana
No comments: