Mashabiki wa Arsenal wanasubiri uzinduzi wa jezi mpya za klabu yao wiki ijayo, lakini kwa bahati mbaya au nzuri zimevuja. Mtumiaji wa akaunti ya Twitter, @oitzbrad ametweet picha hizo chini zinazoonyesha jezi za Arsenal za msimu ujao.
Ni wiki iliyopita tu kiungo wa Gunners, Mesut Ozil alipigwa picha nje ya nyumbani kwake mjini London akiwa ameshika jezi namba 11 ya timu hiyo iliyotengenezwa maalum kwa ajili ya mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ujerumani.

No comments: