Jeshi la polisi wilayani Nzega mkoani Tabora limemkamata mbunge wa jimbo la Nzega Dkt. Hamis Kigwangalla aliyekuwa kwenye maandamano ya wachimbaji wadogo wa dhahabu ya kupinga kufungwa kwa machimbo yao ya mwashina yaliyo jirani na mgodi wa Resolute Tanzania limited. Kabla ya kukamatwa kwa mbunge huyo askari wa jeshi hilo wametumia mabomu ya machozi na silaha za moto kuwatawanya wachimbaji hao wadogo waliokuwa wamemzunguka mbunge huyo ili asikamatwe.
Awali mbunge huyo amefanya mkutano mkubwa wa hadhara na wachimbaji hao katika kijiji cha Nzega ndogo wilayani humo ambapo ameelezwa matatizo ya kufungwa kwa machimbo hayo na kamishna wa madini nchini bw. Paulo masanja bila kujali gharama walizoingia wachimbaji hao wadogo kwenye eneo hilo. Kufuatia hali hiyo Dkt. Kigwangalla amewataka wachimbaji hao kudai haki yao kwa kufuata taratibu zinazostahili bila kujali tofauti zao kisiasa, kikabila na kidini na badala yake wawe kitu kimoja na kuwa japo eneo hilo liko ndani ya leseni ya mgodi wa resolute lakini mgodi huo hauna uwezo wa kuchimba dhahabu kwa kuwa ardhi hiyo ni ya wananchi ambao hawajalipwa fidia.
Hivi ndivyo Mbunge wa jimbo la Nzega mkoani Tabora Dkt Hamis Kiwangala
No comments: