Ilipoishia
Johnson aliwahi asubuhi kama kawaida yake akaanza kujiandaa kwa ajili ya kwenda gengeni kwake akamwambia Maria awahi kwenda kwao kabla wazazi wake hawajarudi
Johnson aliwahi asubuhi kama kawaida yake akaanza kujiandaa kwa ajili ya kwenda gengeni kwake akamwambia Maria awahi kwenda kwao kabla wazazi wake hawajarudi
Endelea
Johnson aliondoka huku anamsisitizia sana Maria asibaki pale nyumbani kwake asubuhi ile ile ajiandae arudi nyumbani kwao akaondoka akamuacha Maria bado kalala. Alifika gengeni kwake akafungua akaanza kupanga panga bidhaa zake alivyomaliza akachukua simu yake akampigia Maria akamuuliza "vipi mpenzi wangu umeshaondoka? Maria akamjibu "bado nipo kwako mpenzi ila nimempigia housegirl simu kaniambia nyumbani kupo shwari wala hamna tatizo"
Johnson alikasirika sana kusikia vile akamwambia Maria "hata kama umempigia mfanyakazi wenu simu we jiandae uondoke hapo usije ukaniletea matatizo mimi wazazi wako wanaweza kurudi muda wowote, nenda kwenu uje siku nyingine" Maria alivyoona Johnson kabadilika akamwambia "sawa mpenzi nimekubali naenda nyumbani ila nikiona hadi jioni wazazi wangu hawajarudi nitakuja tena kulala na wewe huku kwako"
Johnson akamwambia "we katulie kwanza mimi najua hapo wazazi wako wamekutega tu hawawezi kukuambia watarudi lini wala saa ngapi wanataka wakustukize sasa ukija kulala huku wakirudi ghafla wakute hujalala kwenu itakuwa balaa" Johnson alimuelewesha Maria hadi akamuelewa yeye akaendelea na shughuli zake huku akiwa na amani sababu Maria alimsikiliza alivyomwambia arudi nyumbani kwao. Mzee Joseph alienda kukaa na Johson pale gengeni kwake wakawa wanapiga stori akamuuliza Johnson "vipi yule mpenzi wako sasa hivi mnaenda sawa? Johnson akaguna akamjibu "Yani mzee nakushukuru sana kwa yale maneno uliyompa siku ile hapa gengeni sasa hivi kidogo kajirekebisha hanifuaati tena hapa gengeni kwangu hata nyumbani kwangu haji hovyo ile jana ndo ilikuwa majanga" Mzee Joseph akamuuliza Johnson Majanga gani tena kijana wangu?
Johnson akamwambia "jana muda ule natoka huku gengeni usiku ule nilimkuta nyumbani kwangu kalala nilichanganyikiwa nilivyomuuliza kwanini yupo pale usiku wote ule akanijibu wazazi wake hawapo wamesafiri wameenda msibani nikalala naye ila nimemwambia arudi kwao mapema kabla wazazi wake hawajarudi" Mzee Joseph akacheka sana akamwambia Johnson "we kijana sijui umempa nini yule binti yani na uzuri wake wote ule na elimu yake na utajiri wa kwao lakini kafa kaoza kwako wewe muuza genge una bahati sana kijana wenzako hizo bahati wanazitafuta kila kukicha hawazipati sasa inabidi umtumie vizuri yule binti atakutoa kimaisha."
Johnson alishtuka kidogo akamuuliza mzee "mbona sijakuelewa mzee atanitoa kimaisha kivipi?
Mzee akacheka akamwambia "hapa mjini kijana wangu watoto wa kishua kama wale wanaweza wakakufanya uache kuuza genge hapa ufanye biashara kubwa wanaweza wakakufanya uwe na pesa kupitia zile zile pesa za nyumbani kwao." Johnson akabaki tu anamuangalia mzee Joseph alikuwa hajamuelewa alivyomuambia Maria anaweza akamfanya awe na pesa akamuuliza yule mzee "Mzee Joseph mbona sijakuelewa atanifanya niwe na pesa kivipi? Mzee akacheka kidogo akamuambia "Yule mpenzi wako kwao wana pesa sana na ukiangalia yeye anasoma na umesema wazazi wake wanampenda sana na kumsikiliza na yule kwako amekufa ameoza yani anakupenda sana kwa hiyo wewe hata leo hii ukimuambia akusaidie laki mbili uongezee mtaji kwenye hili genge lako lazima tu atafanya juu chini pale kwao atadanganya chochote ili tu akupe wewe hiyo pesa"
Johnson alimsikiliza mzee Joseph kwa makini akaguna akamwambia "mzee mimi naogopa sana tangu nizaliwe sijawahi kumuomba mwanamke hela mimi nna aibu sana"
Mzee Joseph akamwambia "acha ujinga wewe aibu mbele ya pesa yani wewe huyo mwanamke uliyenaye angempata mwanaume mjanja angemtumia vizuri sana yule binti kwao hamna shida sasa wewe kama unamuonea aibu wakati ni mpenzi wako anakupenda hasikii wala haoni utauza genge hapa hadi uzeeke" Johnson aliyafikiria sana yale maneno ya mzee Joseph sababu yeye na Maria walikuwa wapenzi wa mda mrefu lakini hata siku moja hakuwahi kumuambia Maria shida zake japo siku mara nyingi maria alikuwa anamnunulia zawadi kibao kama nguo na baadhi ya vitu vya ndani kwake. Johnson akamuambia yule mzee "Sasa mzee Joseph wewe jifikirie yule Maria yeye ni mwanafunzi hafanyi kazi yoyote sasa mimi nitamuomba vipi hela na ukiangalia bora mimi hata nauza hapa genge napata pesa ndogo ndogo za kula." Mzee akamwambia "yule hata kama anasoma lazima atakuwa na pesa tu wewe jaribu siku kumuomba pesa utakuja kuniambia au kama wewe unamuogopa huyo mpenzi wako siku akija hapa gengeni kwako njoo unistue uone mimi mzee mzima nitakavyompanga hapa hadi akuongezee mtaji kwenye hichi kigenge chako ndio utajua hadi mimi mzee mzima nimekuzidi maujanja"
Johnson alicheka sana kusikia vile akamuambia mzee "sawa mzee siku Maria akija hapa gengeni nitakuita nije nione hayo maujanja yako ambayo utampa mpenzi wangu hadi aniongezee mtaji"
Mzee Joseph na Johnson walipiga stori walivyomaliza maongezi yao mzee Joseph akaondoka zake akamuacha Johnson pale gengeni kwake. Maria alimpigia simu Johnson akamuambia "bby mimi nimerudi nyumbani nimekuta pako salama wazazi wangu bado hawajarudi nimempigia mama simu ameniambia wanarudi kesho jioni kwa hiyo badae tena nakuja kulala nyumbani kwako"
Johnson akamwambia "Maria mpenzi wangu nakuomba leo usije kwani jana hujaridhika tulivyolala wote kuwa makini mpenzi utanisababishia matatizo wazazi wako wanaweza wakawa wamekutega tu wamekuambia wanakuja kesho jioni kumbe wapo njiani muda huu wanarudi wasije wakakukosa hapo ukanisababishia mimi matatizo"
Maria akamwambia "Mpenzi wangu punguza uoga wazazi wangu mimi nawajua hawawezi kunidanganya mimi sijaridhika nilivyolala huko kwako jana na leo nataka nije alafu nataka tuongee vitu vingi sana"
Itaendelea.......................
No comments: