Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa
Morogoro Mh Abdalah Shaweji Akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya
kuwasili Ofisi za CCM Wilaya ya Mvomero
Wajumbe
wa Kmatai ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro
Wakisaini kitabu cha wageni kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Mvomero.
Katibu
wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro Mh Abdalah Shaweji aliyevaa
Miwani Akipatiwa maelezo kuhusu kilimo cha Mpunga kutoka kwa Mkuu wa
Chuo cha Mkindo kata ya Hembeti Wilaya ya Mvomero ikiwa ni Maadhimisho
ya Siku ya Jumuiya ya wazazi.
Katibu
wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro Mh Abdalah Shaweji Akiwahutubia
wananchi wa kata ya Hembeti waliojitokeza kwa wingi katika Sherehe za
Umoja wa wazazi Mkoa wa Morogoro Ambapo katika Hotuba yake Aliwataka
wana CCM Kushirikiana kwa Pamoja Katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
vitongoji na Vijiji.Pia Alisisitiza Msimamo wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa
Morogoro ni kwamba Katika Katiba Mpya wanaunga Mkono Msimamo wa Chama
cha Mapinduzi wa Serikali Mbili na Kuwaomba wananchi Mara baada ya
Rasimu ya Mwisho Kuja waichague serikali Mbili katika Kura ya Maoni ya
Kupitisha Katiba Mpya.
Katibu
wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro Mh Abdalah Shaweji Akipanda
Miti katika Maazimisho ya Sherehe za Jumuiya ya Wazazi
Wapenzi
wa Chama cha Mapinduzi CCM Kutoka Wilaya ya Mvomero wakiwa wamejitokeza
kwa Wingi kwenye Maadhimisho ya Siku ya umoja wa Wazazi Kimkoa ambayo
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro Mh Abdalah Shaweji Alikuwa
Mgeni Rasmi kwa niaba ya Mwenyekiti wa Umoja huo.
Wanachma wapya wa chama cha Mapinduzi wakiapa Mbele ya Mgeni Rasmi mara baada ya kukabidhiwa kadi.
No comments: