Majaji
wa Shindano la Kusaka Vipaji vya Uigizaji Tanzania lijulikanalo kama
Tanzania Movie Talents, Single Mtambalike (kulia), Yvonne Chery
(Katikati) na Roy Sarungi (Kushoto) wakipitia alama za washiriki
kwaajili ya kuweza kuwatangaza washindi waliofanikiwa kuingia hatua ya
tatu ambapo wanachukuliwa washiriki 30 kwaajili ya kupata mchujo wa
washindi watatu bora ambao wataibuka na Kitita Cha Shilingi laki 5 kila
Mmoja kwa Kanda ya Ziwa na baadae kujiunga na washindi wengine watatu
kutoka kila kanda katika fainali ya mwisho itakayofanyika Mkoani Dar Es
Salaam na Mshindi Kujinyakulia Zawadi Kubwa kabisa ya Kitita Cha
Shilingi Milioni 50 za Kitanzania. (50,000,000/=)
Baadhi ya washiriki wakionyesha uwezo wao wa kuigiza mara baada ya kupewa muswada (script).
Baadhi
ya washiriki wakiwa mbele ya majaji (hawapo pichani) kwaajili ya
kutajwa washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya tatu ambapo washiriki
30 tu ndio watachukuliwa kwaajili ya kupatikana washindi watatu
watakaoibuka na kitita cha Shilingi laki 3 kila Mmoja na Baadae kuungana
na washindi wengine wa kanda zilizobakia katika Fainali ya mwisho
itakayofanyika Mkoani Dar Es Salaam.
Baadhi
ya washiriki wawili (wa kwanza kulia na wapili) wakiwa hawaamini kama
wamechaguliwa kuingia hatua ya washiriki 30 kwaajili ya mchujo wa kupata
washindi watatu wa Kanda ya Ziwa, Mkoani Mwanza
Mmoja
wa washiriki aliyefanikiwa kuchaguliwa kwa hatua ya tatu (mwenye fulana
nyeupe) akipongezwa na mshiriki mwenzie ambae hakupata bahati ya
kuchaguliwa kwaajili ya kuendelea na hatua inayofuata.
Washiriki wakipongezana mara baada ya kuchaguliwa kuendelea na hatua inayofuata.
Baadhi
ya washiriki waliofanikiwa kuchaguliwa kwa hatua ya tatu wakishangilia
mara baada ya kuchaguliwa.
Picha na Josephat Lukaza wa Proin Promotions
Limited - Mwanza
No comments: