Kinana akilakiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma, Walidi Kaburu baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma.Kulia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka Zanzibar, Ally Karume.
Gwaride la Vijana wa CCM, likiwa tayari wakati wa mapokezi hayo ya Kinana.
Kinana akivishwa skavu na kijana Hadja Kanyoe wakati wa mapokezi
Vijana wa CCM wakimpigia makofi Kinana uwanjani hapo
Kinana akisalimiana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye aliyfika kumlaki uwanjani hapo na kuungana naye kwenye ziara ya mkoa huo na wa Katavi.Nape alikuwa Chalinze ambako alikuwa Mratibu Mkuu wa Kampeni za Uchaguzi mdogo wa ubunge wa Jimbo la Chalinze ambapo Ridhiwani Kikwete wa CCM ameibuka mshind na kuvibwaga kwa mbali vyama vingine vya upinzani.
Kinana akiwa na viongozi wa CCM Mkoa wa Kigoma pamoja na Mkuu wa Mkoa huo, Kanali mstaafu Issa Machibya waliofika kumlaki uwanjani hapo.
Nape akielezea jinsi CCM ilivyoshinda kwa kishindo katika chaguzi za Chalinze, Kalenga na madiwani wakati wa mkutano wa Halmashauri ya Mkoa wa Kigoma
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kigoma wakisikiliza kwa makini wakati Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akizungumza nao baada ya kupewa taarifa ya mkoa huo.
Kinana akizungmza katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kigoma kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoa wa Kigoma.
Nape akigalia mawe yanayotumika kujengea mabanda ya maduka yanayojengwa na CCM Mkoa wa Kigoma
No comments: