Manchester United imeaga Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufungwa mabao 3-1 na wenyeji Bayern Munich Uwanja wa Allianz-Arena mjini Munich, Ujerumani usiku huu. Hiyo inamaanisha United imeaga kwa kipigo cha jumla ya mabao 4-2, baada ya awali kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester.
United leo ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 57, mfungaji beki wake Mfaransa, Evra.
Sekunde 22 baadaye Mcroatia, Mandzukic akaisawazishia Bayern akitumia fursa ya wachezaji wa United kuzubaa kwa furaha ya bao.
Bao hilo liliwaondoa mchezoni United na kuanza kufanya madudu, hali ambayo iliwapa fursa mabingwa hao wa Ulaya kupata mabao mawili zaidi.
Muller alifunga la pili dakika ya 68 pasi ya Robben ambaye alikuwa mwiba mchungu kwa Mashetani hao Wekundu usiku huu.
Arjen Robben akafunga mwenyewe bao la tatu kwa shuti la mbali dakika ya 76 na kuzima kabisa ndoto za kocha David Moyes kufanya maajabu kwenye michuano hiyo ya Ulaya

No comments: