Maandamano yakiwa yameanza kuelekea ukumbi wa Mlimani City
Mmoja ya Waandamaji wa siku ya kumbukumbu ya mauaji ya Rwanda ikiwa imetimia Miaka 20 akiwa amebeba Mwenge Maalum kwa ajili ya Maadhimisho.
Maandamano ya Kumbukumbu ya miaka 20 ya Mauaji ya Kimbari yaliyotokea mwaka 1994 yakiendelea kuelekea Ukumbi wa Mlimani City kwa ajili ya Maadhimisho hayo.
Baadhi ya Wanafunzi pamoja na watu wengine mbalimbali wakiwa wameshika mabango mbalimbali yanayo elezea siku ya kumbukumbu ya Mauaji ya Rwanda yaliyotokea Mwaka 1994
Maandamano yakiwa yamewasili nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City kwa ajili ya kukabidhi Mwenge huo kwa Mgeni rasmi Mh. Profesa Mark J. Mwandosya Waziri Ofisi ya Rais.
Mgeni Rasmi Mh. Profesa Mark J. Mwandosya Waziri Ofisi ya Rais akipokea Mwenge Maalum wa Kumbukumbu ya Miaka 20 ya Mauaji ya Rwanda kutoka kwa Mustapha Issa wa kwanza kutoka upande wa kushoto pamoja na Amina Mtegeti.
Mshehereshaji wa maadhimisho ya kumbukumbu za Miaka 20 ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda Usia Nkhoma Ledama kutoka UNIC Dar es Salaam, akizungumza jambo kwenye sherehe hizo.
Baadhi ya wageni waliofika katika kumbukumbu hizo wakiwa wanaimba nyimbo mbili za Taifa kutoka Rwanda na Tanzania.
Baadhi ya waliofika katika Kumbukumbu za Miaka 20 ya mauaji
Mchungaji Safari Paul akiendesha Maombi Maalum kwa ajili ya Kumbukumbu ya Miaka 20 ya Mauaji ya Rwanda ambapo zaidi ya watu Milioni Moja waliuawa.
Sheigh Othman akiomba dua Maalum kwa ajili ya Miaka 20 ya kumbukumbu ya Mauaji ya Rwanda.
Mgeni Rasmi Mh. Profesa Mark J. Mwandosya Waziri Ofisi ya Rais akipokea Mwenge Maalum wa Kumbukumbu za Miaka 20 ya Mauaji ya Rwanda kwa ajili ya kuwasha Mishumaa ili kuwakumbuka wale wote waliopoteza Maisha.
Akiwasha Mshumaa kwa ajili ya kumbukumbu ya Miaka 20 ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda.
Aliyekuwa katibu Mkuu wa Saba wa Umoja wa Afrika Dk. Salim Ahmed Salim akiwasha Mshumaa kwa ajili ya Kumbukumbu ya Miaka 20 ya mauaji Kimbari ya Rwanda.
Mmoja wa wahimizaji wa Amani na Upendo Amina Mtengeti akiwa anazungumza Jambo wakati wa Maadhimisho ya Miaka 20 ya kumbukumbu ya Mauaji ya Rwanda.
International Criminal Tribunal for Rwanda (ICTR) Registrar, Ndugu Bongani Majola akizungumzia kwa kifupi juu ya Mauaji ya Rwanda ambapo sasa ni Miaka 20 tangu yalipo tokea
Wanafunzi wakiimba wimbo maalum kwa ajili ya kumbukumbu ya Mauaji ya Rwanda
Mwakilishi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon , Mh. Dk Jamal Gulaid akisoma Ujumbe wa Katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa.
Mh. Benjamin Rugangazi akitoa Neno kutoka Ubalozi wa Rwanda Nchini Tanzania
Zainab Abdallah kutoka Youth of United Nations akisoma Shairi maalum wakati wa kumbukumbu za Miaka 20 ya mauaji ya Rwanda.
Zainab Abdallah kutoka Youth of United Nations akisoma Shairi maalum wakati wa kumbukumbu za Miaka 20 ya mauaji ya Rwanda.
Mgeni Rasmi Mh. Profesa Mark J. Mwandosya Waziri Ofisi ya Rais akitoa hotuba yake kwa wananchi waliofika katika Maadhimisho hayo ya Miaka 20 ya Mauaji ya Rwanda.
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Swaumu Vuzzo akitoa neno la Shukurani kwa wageni waalikwa waliohudhuria maadhimisho hayo.
Baadhi ya mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania, wadau mbalimbali wa mashirika ya Kimataifa na Sekta binafsi waliohudhuria maadhimisho hayo.
No comments: