Mwakilishi
wa Jimbo la Kiembe samaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (wakatikati)
wakiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Jimbo la Kiembe samaki Ramadhan
Mrisho wa kushoto, kulia Mwenyekiti wa Kamati ya michezo ya Jimbo hilo
Juma Abdul-rabi kabla ya kukabidhi pesa taslim na vifaa vya michezo kwa
tim za Jimbo hilo ikiwa ni ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni zake hafla
hiyo imefanyika katika Hoteli ya Ocean View Mjini Zanzibar.
Baadhi ya wanamichezo na viongozi mbalimbali wa Jimbo la Kiembe samaki wakimsikiliza Mwakilishi wa Jimbo hilo Mhe. Mahmoud Thabit Kombo kabla ya kukabidhi pesa na vifaa vya michezo kwa timu za Jimbo lake.
Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi pesa Tsh. laki nne kiongozi wa tim ya Smoll Zico ya Kiembe samaki ikiwa ni ahadi aliyoito wakati wa kampeni zake.
Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi Katibu wa Tim ya Mbweni Kids Khalifa Khamis vifaa mbalimbali vya michezo, Jumla ya tim nane za Jimbo hilo zimepata pesa na vifaa mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya shiling milioni saba na nusu.
No comments: